C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

ITAZAME HAPA BRAND NEW JOINT FROM CHEGE FT DIMOND PLATNUM WAACHE WAOANE

UONGOZI WA CLUB YA MADRID WAANZA KUMJADILI ZINEDINE ZIDANE.......................................

Club ya Real Madrid chini ya raisi wa klabu hiyo Florentino Peres imeanza mchakato wa kumjadili kocha wa muda wa club hiyo zinedine zidane aliyepewa timu baada ya kocha Rafael Benitez kufutwa kazi ya kukinoa kikosi hicho cha mabigwa wa UEFA champions league, wenye mskani yao katika jiji la madrid nchini Uhispania. 
Uongozi wa club hiyo umeanza kumjadili kocha huyo, ili kuangalia uwezekano wa kumpa mkataba wa kudumu wa kukinoa kikosi hicho cha real madrid,baada ya kuiongoza timu hiyo kwa mafanikio katika msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa kombe la club bigwa barani ulaya maarufu kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE......

ZIMESALIA SIKU KUMI KABLA YA KUANZA TENA KWA MSIMU WA LIGI KUU NCHINI WINGEREZA[ EPL]..........,,,,,

Zimebaki siku kumi pekee kabla ya kuanza tena kwa msimu mpya wa English premier League[EPL] ya nchini wingereza ,amabapo kwa msimu huu ligi hiyo inatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na kua na makocha wenye viwango vya juu katika ufundishaji wa soka.
Miongoni mwa makocha hao wanaotarajiwa kuleta upinzani wa hali ya juu katika ligi hiyo nchini wingereza ni pamoja na Jose Morinho wa Manchester united, Pep Guardiola wa Manchester city, Antonio conte wa Chelsea pamoja na Jorgen Klopp wa Liver pool.

CLUB YA ARSENAL YAINGILIWA NA MAHASIMU WAO KATIKA DILI LA USAJILI...............

Washika bunduki wa kaskazini mwa jiji la London [ARSENAL] wamewasilisha maombi kwenye klabu ya Valencia na West Brom, wakitaka kuwa sajili shrodran mustafi na jonny Evans.
Arsenal wamewasilisha maombi hayo, lakini hawajaweka mezani dau kwa wachezaji hao wawili.
Huenda the Gunners wakapata upinzani mkali kutokakwa chelsea ambao wameonyesha nia ya kumsajili Mustaki ambaye aliwahi kuitumikia Klabu  ya Everton.
Mkataba wa Beki huyo kutoka nchini ujerumani unaonyesha kuwa  kama kuna klabu ikitaka kumsajili inatakiwa kutoa kiasi cha paundi milioni 41, lakini Valencia wamejishusha na kuwa tayari kupokea hadi pauni million 25.
Arsenal wanahitaji kuongeza beki mpya baaada ya nahodha wao per mertasecker  kusumbuliwa na majeraha amabayo huenda yakamweka nje hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Beki huyo wa ujerumani alipata majeraha hayo wakati wa mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya RC lens, ambapo  ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

KIUNGO PAUL POGBA AMKABITHI MSANII DRAKE JEZI YA JUVENTUS YENYE JINA LAKE..................

Mchezaji Paul Pogba ameleta Headlines mpya baada ya kumkabithi msanii Drake jezi no 10 ya Juventus yenye jina la POGBA,

Alhamisi, 28 Julai 2016

NEW HIT FROM KALA JEREMIAH FT MIRIUM CHIRWA WANANDOTO WATCH IT HERE............................

KOFFIE OLOMIDE ATUPWA JELA MIEZI 18 MJINI KINSHASA NCHINI CONGO............

Mahakama mjini kinshasa imemuhukumu mwanamuziki Mkogwe Koffie Olomide kwenda jela miezi 18 kwa kosa la kumpiga mngenguaji wake kudhalilisha utu wa mwanamke.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi mjini humo imemtaja mkogwe huyo kama sugu wa makosa hayo ambayo amekua akiyatenda mara kadhaa
Msanii huyo ameanza kutumikia adhabu yake katika gereza moja nchini humo na wakati akiingia kwenye gereza hilo Koffie alisikika akisema siwapendi wanawake,

KLABU YA VILLARREAL YAKAMILISHA USAJILI WA MSHAMBULIAJI KUTOKA CHELSEA......................................

Klabu ya Villarreal ya nchini Hispania imedhibitisha kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Brazil ,Alexandre pato
Villarreal wamekamilisha usajili wa mshambuliaji huyo ambae mwanzoni mwa mwaka huu alisajiliwa kwa mkopo na klabu ya chelsea yanchini wingereza akitokea Corithians ya nchini Brazil.
Taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya klabuhiyo ya El Madrigal zimeeleza kuwa pato amesaini mkataba wa miaka minne.
Hata hivyo haikuelezwa ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kama ada ya usajili wa mshambuliji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye aliwahi kutamab na klabu ya AC milani ya nchini italia kuanzia mwaka 2007-2012.
Klabu ya sevilla cf ya nchini Hispania nayo ilikua inahusishwa na kutaka kumsajili Pato.

HATMA YA SAKATA LA KIUNGO PAUL POGBA KUTUA OLD TRAFORD KUJULIKANA NDANI YA SAA 48 ZIJAZO............

Sarakasi za usajili wa kiungo kutoka ufaransa [PAUL POGBA]hatma ya uhamisho wa mchezaji huyo kujulikana ndani ya saa 48.
Klabu hiyo ya manchester united yenye maskani yake katika jiji la Manchester nchini Wingereza inatarajia kukamilisha dili la kumsajili kiungo huyo kutoka Nchini Ufaransa na klabu ya Juventus ya nchini italia Paul pogba ndani ya saa 48 zijazo.
Man united wanatarajia kukamilisha dili hilo kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya dunia, ambayo kwa sasa inashikwa na mshambuliaji kutoka Nchini wales na klabu ya Real madrid Gareth Bale.
Mashetani hao wekundu tayari wameshawasilisha ofa ya pauni milioni 100, huko Juventus stadium na baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa uongozi wa mabigwa wa soka nchini Italia Juventus umeshakubali.
Jambo lingine ambalo linaonyesha dalili za dili la wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda likakamilishwa ndani ya saa 48 zijazo ni mazungumzo ya uhamisho huo kati ya wakala wa Pogba Mino Raiola, na Mkurugenzi wa club hiyo ya Juventus Giusppe Beppe Moratta.
Mwanzo wawili hao walikua wakipingana kuhusu swala la uhamisho wa mchezaji huyo.

RAPA NAY WA MITEGO ADAI ATAWAMIS......

Rapa Nay wa mitego ambae amefungiwa kujihusisha na shuhuli za muziki na Baraza la sanaa nchini BaSATA, amefunguka na kudai kuwa atazimiss shuhuli alizokua anazifanya.
Kupitia ukurasa wake wa istagram, rapa huyo ameweka picha akiwa jukwaani na kuandika ujumbe uliosomeka "daa nitazimiss sana hizi.
Basata imemfungia rapa huyo kwa kipindi amabacho hakijajulikana, mpaka pale watakapojiridhisha kwamba amebadilika ikiwemo kujisajili kufanya shuhuli za sanaa nchini.

Jumatano, 13 Julai 2016

KLABU YA CHELSEA YAZINDUA RASMI JEZI ITAKAYOTUMIKA KATIKA MSIMU UJAO WA LIGI KWA MECHI ZA UGENINI...........

klabu ya chelsea yenye maskani yake jijini london nchini wingereza yazindua rasmi jezi itakayo tumika katika mechi zake za ugenini.
klabu hiyo amabyao kwa sasa inaongozwa na kocha mpya Antonio conte baada ya kutimuliwa kwa kocha wa awali Jose morinho ipo katika maandalizi ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu nchini wingereza, imezindua rasmi jezi hiyo itakayo tumika  katika mechi zake zote za ugenini kwa msimu ujao wa 2016-2017...

ITAZAME HAPA BRAND NEW JOINT FROM DIMOND PLATNUM FT P SQUARE KIDOGO OFFICIALY VIDEO......................

MAMA WA CRISTIANO RONALDO AMJIA JUU MCHEZAJI WA UFARANSA DIMITRI PAYET......................................

Mama wa Cristiano Ronaldo Dolores Aveiro amjia juu Dimitri payet,kufuatia rafu mbaya aliyomchezea mwanae katika fainali ya EURO 2016  Nchini Ufaransa.
Malalamiko hayo yametolewa na mama mzazi wa cristiano Ronaldo,baada ya mwanae kuumia katika fainali ya kombe la michuano ya mabara ya ulaya UEFA EURO, ambapo katika mchezo huo wa fainali uliwakutanisha Timu ya taifa ya ureno dhidi ya Ufaransa waliokua wenyeji wa michuaano hiyo, ambapo katika kipindi cha kwanza mchezaji huyo aliumia baada ya kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa ufaransa Dimitri payet hali iliyopelekea mchezaji huyo kushindwa kuendelea na mchezo,huyo na kutolewa nje ya uwanja huku akitokwa machozi, hali iliyopelekea mama mzazi wa mchezaji huyo kuja juu na kudai kua mchezaji huyo wa ufaransa Dimitri Payet alikusudia kumchezea mwanae rafu hiyo kwa kuandia katika ukurasa wake katika mtandao wa twiter  ''to play football is to kick a ball and not to kick the legs,,aliandika mama huyo.
Hata hivyo mechi hiyo iliisha kwa timu ya Taifa ya Ureno kufanikiwa kutwaa ubigwa wa michuano hiyo kwa kufanikiwa kuifunga Ufaransa goli  moja kwa sifuri goli lililofugwa na mchezaji Heder katika dakika 30 za nyongeza baada ya kukamilika dakika 90 za kawaida bila mshindi kupatikana.

THIERY HENRY AAMUA KUACHANA NA KAZI YA UKOCHA KATIKA CLUB YA ARSENAL.......................................

Gazeti la The sun linaripoti kuwa Thiery Henry ameachanana kazi ya ukocha wa muda wa timu ya vijana ya Arsenal baada ya kupishana kauli na meneja Arsener Wenger kufuatia kazi yake ya uchambuzi wa masuala ya soka kwenye Television.
Thiery Henry alikua anafanya kazi kwa part time na Arsenal ,kama kocha wa vijana chini ya umri wa miaka 18,alipata leseni ya UEFA  wakati huohuo akiwa ni mchambuzi wa kituo cha Television cha Sky sport, Henry aliomba kupewa mkataba wa kufanya kazi na Arsenal kwa msimu unaokuja kwa malipo kidogo, lakini boss wake Arsenel wenger alimpa mashsrti ya kufanya kazi hiyo kwa kumwambia kama anataka kazi hiyo basi aachane na kazi ya sky sports na kama anataka kazi Sky sport basi aachane na Arsenal.
Maamuzi aliyofanya Henry ambae ni gwiji wa soka wa zamani wa club hiyo yenye maskani yake katika jiji la London nchini wingereza, ameamua kuacha kazi katika Club hiyo na kubaki kuwa mchambuzi katika kituo cha Television cha Sky sport.
Maamuzi hayo yaliyofanywa na Gwiji huyo yamewafurahisha baadhi ya viongozi wa club hiyo ya Arsenal..

Ijumaa, 8 Julai 2016

MAMIA YA WATU WATAPIGWA PICHA ZA UTUPU KATIKA MJI WA HULL NCHINI UINGEREZA.........................

Mamia ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherekea utamaduni katika mji wa Hull, uingereza.
Tukio hilo litakuwa la kusherekea mji huo kama mji wa utamaduni.
washiriki watapakwa rangi ya samawati jumamosi na kisha wapigwe picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa nampiga picha spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya sanaaa ya Ferens Art Gallery.
picha zitakazopigwa zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
Tunick, anayetoka New York, amewahi kufanya kazi kama hiyo kwingine.
 Amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi sydney opera House, place des Art mjini Montrel, Mexico city na mjini Munich nchini  Ujerumani.
Bw Tunick amesema kazi zake'' hugusia historia ndefu ya sanaaa ya utupu''
''Mavazi ni sanaa ya mtu mwingine''anasema.
Fashion ni sanaa. kwa kuondoa hilo[ mavazi] nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi wake''
Watu karibu 2000 wamejiandikisha kupigwa picha tangu wazo hilo litangazwe mwezi machi.
Baraza la mji wa Hull limesema baadhi ya barabara zitafungwa wakati wa shuhuli hiyo jumamosi asubuhi.

PAUL POGBA AKIRI KUA ANAHITAJI KURUDI KATIKA CLUB YA MANCHESTER UNITED.......

Jarida maarufu huko nchini ufaransa L ,Eguipe limedai  kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Paul pogba amewaambia marafiki zake na wachezaji wenzake kwamba anataka kurejea Man United ikiwa ni Miaka minne tangu aondoke Old Trafford kwenda kujiunga na klabu ya Italy Juventus.

Jumatatu, 4 Julai 2016

MABASI MAWILI YA CITY BOYS YAUWA 24 MKOANI SINGIDA...

Mabasi ya  City boys yanayofanya safari zake kutoka dar es salam ,mwanza,na Shinyanga Dar es salam, yamepata ajali katika eneo la Miwani mkoani Singida na watu 24, wamepoteza maisha papo hapo na wengine wamejeruhiwa vibaya,baada ya kugongana uso kwa uso..

MANCHESTER UNITED WAPO TAYARI KULIPA PAUNDI MILIONI100 KWA JUVENTUS............

Manchester united wamewaambia juventus kuwa wako tayari kulipa pauni million 100 kumsajili kiungo kutoka ufaransa paul pogba 23,na watampa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.

HAYA NDIO MANENO ALIYOYASEMA BARAKA THE PRINCE, KUMUHUSU MSANII MWENZAKE YOUNG KILLA.

Msanii Baraka the prince, amesema kua hajawai kuzipenda nyimbo za msanni mwenzake Young killa, na wala hategemei kuzipenda nyimbo za msanii huyo mwenzake,
MSanii huyo ametoa maneno hayo wakati akiwa anafanya mahojiano na kituo kimoja cha redio
Hata hivyo kauli hiyo imeonekana kupokewa katika mtazamo tofauti na mashabiki wa mziki wa kizazi kipya, wengi wameonekana kumponda msanii huyo kwa kauli hiyo aliyoitoa na kusema, young kila ni msanii mkubwa na mwenye kipaji cha aina yake, hivyo Baraka the prince bado ni msanii mchanga sana  katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya hivyo hawezi kushindana na young killa.

Jumatano, 29 Juni 2016

ANGALIA NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA BILL NASS CHAFU POZI....................

ANGALIA NA DOWNLOAD HAPA VIDEO MPYA YA BEN PAUL MOYO MASHINE..............

SIKILIZA NA DOWNLOAD NYIMBO YA PAPA WEMBA FT DIMOND PLATNUMZ CHACUN POUR SOI

ANGALIA HAPA VIDEO MPYA YA MR BLUE FT ALLY KIBA MBOGA SABA,,,OFFICIALYNEW VIDEO OF MR BLUE FT ALLY KIBA MBOGA SABA..



CLUB YA CHELSEA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO KUKAMILISHA USAJILI WA MSHAMBULIAJI KUTOKA OLYMPIC MARSEILLE YA NCHINI UFARANSA

Club ya Chelsea yenye maskani yake jijini london nchini Wingereza ipo katika hatua za mwisho kumsajili Mshambuliaji kutoka club ya Olmpic Marseille, Batshuayi kwa ada ya Euro  million 33.
Mshambuliaji huyo ambae ni raia wa Ubelgiji anatarajia kujiunga na hiyo ya chelsea akitokea katika club ya olmpic Marseille ya nchini ufaransa,msimu uliopita mchezaji huyo alifanikiwa kuifungia club hiyo magoli 24 katika ligi ya nchi hiyo maarufu kama League one,.
Mchezaji huyo anatarajia kujiunga na mbelgiji mwenzake Eden hazard katika klabu hiyo ya chelsea katika msimu ujao.
Usajili huo ni wa kwanza kufanywa na club ya chelsea kwa msimu huu chini ya kocha mpya Antonio Conte, ikiwa ni moja ya harakati za kukiboresha kikosi cha club hiyo, kwani msimu uliopita haukua mzuri sana kwa club hiyo, iliyokua ikifundishwa na kocha  jose morinho aliyetimuliwa klabuni hapo baada ya club hiyo kupata matokeo mabaya, kitu kilichopelekea kumaliza katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu nchini wingereza na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya klabui bigwa barani ulaya katika msimu ujao.

CLUB YA LIVERPOOL YAKAMILISHA DILI LA KUMSAJILI MCHEZAJI WA SOTHAMPTON KWA KUMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MINNE.

Klabu ya liverpool  yakamilisha usajili  wa mshambuliaji  Saido Mane,kutoka Sothampthon kwa ada ya Euro million 30.
Mshambuliaji huyo kutoka club ya sothampton anakua ni mchezaji wa pili kuuzwa na club hiyo katika dirisha hili kubwa la usajili wakanza alikua ni Victor wanyama ambae alinunuliwa na club ya Totenham hospurs, yenye maskani yake jijini london nchini wingereza.
Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka minne ambao utamweka klabuni hapo mpaka mwaka 2021,usajili huo ni wa kwanza kufanywa  na klabu hiyo ya liver pool yenye maskani yake katika jiji la liverpool nchini wingereza ikiwa ni moja ya harakati za kuiboresha klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi, kwani itakumbukwa katika msimu uliopita club hiyo ilimaliza ikiwa katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu nchini Wingereza,

Jumanne, 21 Juni 2016

MHARIRI WA GAZIETI LA DIRA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA GAZETI HILO KUTOA HABARI ZISIZO ZA KWELI..

Mhariri wa Gazeti la Dira afikishwa kituo cha polisi baada ya Gazeti hilo kuandika taarifa potofu ya kuibiwa kifaru cha  JWTZ.
Tangu juzi kumekuwapo na taarifa za kuibiwa kifaru cha jeshi la wananchi wa Tanzania Zilizoripotiwa na Gazeti la Dira.
jana JWTZ imekanusha taarifa hizo na kulitaka gazeti hilo kukanusha na kuomba radhi mara moja kwa kutoa taarifa za uongo kwa uma.
Taarifa mpya leo ni kwamba jeshi la polisi nchini linamshikilia mhariri wa Gazeti la Dira kwa mahojiano zaidi.

Alhamisi, 16 Juni 2016

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA RAPPER CHID BENZ KWA SASA BAADA YA KUPATA MATIBABU................

Huu ndiyo muonekano mpya wa sasa hivi wa rapa chid Benz, aliekua akipata matibabu kutokana na kuadhiriwa na dawa za kulevya
Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya nchini afya yake imeonekana kuwa nzuri baada ya kupelekwa Sober House ambacho ni kituo kinachotoa huduma kwa watu walio adhiriwa na madawa ya kulevya , rapper huyo alikaa kituoni hapo na kupatiwa matibabu kwa mwezi mmoja na baadae kuruhusiwa baada ya afya yake kurudi katika hali ya kuridhisha,
Hata hivyo meneja wa kundi la Tiptop connection Babu tale ndiye mtu aliejitolea kwa hali na mali kuhakikisha msanii huyo anarudi katika afya yake ya kawaida na kuweza kuendelea na shuhuli zake za muziki,.
Sambamba na hilo msanii huyo baada ya kupona sasa atakua anasimamiwa  na Meneja Babu tale katiaka kazi zake za mziki kwa sasa.

WABUNGE WA CHAMA CHA MAPINDUZI[ CCM]WAPENDEKEZA KUONGEZWA KWA SHILINGI 50 KATIKA KILA LITA YA MAFUTA....

Wabunge wa chama cha mapinduzi ccm wataka shilingi 50 iongezwe katika kila lita ya mafuta nchini.
Wabunge hao wa chama hicho tawala wamefikia hatua hiyo ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu walipopinga vikali zoezi la kukatwa kodi katika fedha zao za kiinua mgongo [penssen] wakidai kua hawana fedha yoyote wanayoitegemea ili kuendesha maisha yao baada ya kuustaafu tofauti na hiyo na kuongeza kua muda wao wa kukaa madarakani ni miaka mitano peke yake.
wawakilishi hao wa wananchi katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wametoa pendekezo hilo bungeni ikiwa ni zaidi ya mwezi sasa wabunge wa vyama vya upinzani wameweka mgomo wa kuto udhuria vikao vya bunge kwa madai ya kutokua na imani na spika wa bunge hilo la jamuuri ya muungano wa Tanzania.

MUME AMUUA MKEWE KWA KUMNYONGA KWA KANGA KISA WIVU WA MAPENZI......

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rehema Tumbo amenyongwa na mumewe Raphael kazembe tena kwa kutumia khanga mkoani shinyanga kisa kikuu kikiwa ni wivu wa mapenzi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga Graiftoni mushi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na inadaiwa kuwa mwanamke huyo alichelewa kurudi na alipomgongea mumewe chumbani wanakolala hakumfungulia ndipo mwanaume huyo alipoamua kumfuata na kuanza kumpiga na kumnyonga hatimae kumsababishia mauti.
Mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio hili na mpaka sasa polisi wanaendelea na juhudi za kumsaka kokote aliko,mwenyekiti wa mtaa huo bwana Edward Mihayo anasema taarifa zilimfikia kutoka kwa wanamtaa baada ya kushuhudia maiti ya rehema ikiwa imenyongwa kwa kanga.

Jumanne, 14 Juni 2016

ANTONIO KONTE AMTAKA BEKI WA MANCHESTER UNITED MATHEO DAMIAN KATIAKA KLABU YA CHELSEA.......

Kocha mpya wa klabu ya chelsea Antonio Konte  anataka kumsajili beki wa kushoto wa manchester united Mateo Damian,
Kocha huyo mwitaliano  anaetarajia kuanza kazi rasmi katika klabu hiyo yenye maskani yake jijini london nchini wingereza, katika msimu ujao, ameonyesha dhamira ya kutaka kumsajili beki wa pembeni wa manchester united matheo Damiani, beki huyo aliyesajiliwa na klabu hiyo chini ya kocha Luis Vangal, aliyetimuliwa klabuni hapo mwisho wa msimu uliopita,na mikoba yake kuchukuliwa na kocha mreno jose morinho, anauwezekano mkubwa kutua katika klabu ya chelsea kutokana na mahusiano mazuri aliyonayo mchezaji huyo na kocha Antonio Konte,
Kwa sasa mchazaji huyo yupo nhini ufaransa na timu ya taifa ya italy katika fainali za EURO, timu hiyo ipo chini ya kocha antonio konte ambae ni kocha mtarajiwa wa klabu ya chelsea na kuwa pamoja kwa kocha huyo na beki huyo wa mashetani wekundu, huenda ukawa ni mwanya mzuri kwa kocha huyo kumshawishi Matheo Damian kutua Stanford bridger.
Usajili huyo unataka kufanyika ikiwa ni moja ya harakati za kocha huyo mwitaliano  kutengeneza safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya chelsea baada ya kuonekana kutetereka katika msimu uliopita kitu kilichopelekea klabu hiyo ambao walikua ni mabigwa wa tetezi kumaliza msimu wakiwa katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu nchini wingereza...

TMTAZAME HAPA VIDEO YA MCHEKESHAJI STAN BAKORA AKIRUDIA KUIMBA WIMBO WA RAYMOND NATAFUTA KIKI..........................

VIDEO YA STAN BAKORA AKILIIMBA WIMBO WA RAYMOND KWENYE  VIDEO HIII

ITAZAME HAPA NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA MSANII RICH MAVOCO IMEBAKI STORY...............

Jumatatu, 13 Juni 2016

AGALIA HAPA LIVE CONCERT YA MSANII FAT JOE PAMOJA NA FRENCH MONTANA WAKIWA WANA PAFORM LIVE NYIMBO YA AM ALL THE WAY UP.

ANGALIA NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA JAY MOE PESA YA MADAFU,DRAND NEW JOINT FROM JAY MOE PESA YA MADAFU



DONALD TRUMP ASEMA HAYA KUHUSU MAUWAJI YA WATU 50 NCHINI MAREKANI.............

Mwanasiasa wa nchini marekani Donald Trump amesema  mauaji ya watu 50 katika baa jana inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya marekani.

Mwanasiasa huyo amesema hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waislam.
upande wa bi clinton wakiton ambae ni mpinzani wa Donald trump katika kuwania kiti cha uraisi nchini marekani ,wametoa pole kwa waathirika wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Wakati huo,huo shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi wa jinsia moja alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.
Baba Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanae kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaoendeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani sitora yusufiy, amemweleza Mateen kama mtu aliyekuwa na tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini

Alhamisi, 2 Juni 2016

MSANII RICH MAVOCO ASAINI RASMI MKATABA WA KUFANYA KAZI CHINI YA KAMPUNI YA WCB...............

Msanii wa mziki wa kizazi kipya rich mavoko asaini rasmi katika kampuni ya WCB inayomilikiwa na mwanamuziki Dimond Platnum.
Msanii huyo wa kizazi kipya ambae ni mkogwe katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya hapa nchini, amefikia uamuzi wa kusaini katika lebo hiyo ya wasafi baada ya kuridhishwa  na uendeshwaji wa kampuni hiyo iliyochini ya msanii mwenzake Dimond platnum,
Kampuni hiyo ya WCB kabla ya kumsainisha rich mavoco ilikua tayari imeshawasainisha wasanii wengine wawili wanao chipukia ambao ni Harmonize ambae tayari ananyimbo mbili zinazofanya vizuri kwa sasa nyimbo hizo ni  Aiyola,na Bado, huku mwenzake  Raymond akiwa na nyimbo mbili pia ya kwanza inaitwa huku kwetu, na ya pili Natafuta kick.
Mmiliki wa kampuni hiyo ya WCB aliandika haya katika akaunti yake ya facebok huku akiambatanisha na picha hii "welcome rich mavoco  let us take bongo fleva to the world,, aliandika dimond platnum.
Kusainiwa kwa msanii huyo rich mavoco katika lebo hiyo  anakua ndiye msanii wa kwanza mkogwe kusainiwa na lebo hiyo ya WCB..

Alhamisi, 26 Mei 2016

ANTONIO CONTE ACHAFUA HALI YA HEWA NDANI YA CLUB YA CHELSEA.............

Meneja mpya wa klabu ya chelsea Antonio Conte Achafua Hali ya  Hewa Stamford Brigder, baathi ya wachezaji hawajui Hatma Zao,
Majaaliwa ya mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Alexandre Pato ya kuendelea kucheza ndani ya kikosi cha chelsea, yapo mikononi mwa meneja mpya wa klabu hiyo Antonio Conte.
 Wakala wa mshambuliaji huyo aliyesajiliwa huko Stamford Bridger mwezi januari mwaka  2016, Gilmar Veloz amesema mpaka sasa wanasubiri maamuzi ya Conte ambaye yupo na kikosi cha timu ya taifa ya italia kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Euro 2016.
veloz, amesema tumaini lake kubwa kwa mshambuliaji huyo lipo mikononi mwa meneja huyo kutoka  Italia, kutokana na kuamini bado  kuna uwezekano wa pato kuendelea kubaki klabuni hapo.
Amesema anatambua Antonio conte atahitaji kuanza na mipango ya kuwatumia wachezaji atakao wasajili na wale watakaobaki  kikosini, hivyo anaamini pato ni miongoni mwa watakaosubiri kauli ya mwisho ya mwitaliano huyo.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa chelsea wameshajihakikishia nafasi ya kuendelea kubaki klabuni hapo, huku wengine wakitambua fika hawana nafasi ya kucheza soka ndani ya club hiyo ya chelsea.
Mshambuliaji kutoka nchini hispsnia Diego costa anamatumaini makubwa ya kuendelea kusalia kwenye club hiyo, licha kuhusishwa na taarifa za kutakiwa na club yake ya zamani ya Atletico Madrid,huku mshambuliaji kinda Betrand Traore akiwa na matumaini kama hayo kufuatia uwezo wa kufunga mabao manne aliouonyesha wakati wa msimu wa 2015-16.
Mshambuliaji kutoka nchini Colombia, aliyekua akicheza kwa mkopo klabuni hapo Radamel Falcao tayari imeshafahamika anaondoka na kurejea katika klabu yake ya AS monaco ya Ufaransa huku kukiwa na mashaka  kwa mshambuliaji Lic Remy.
Pia kumekua na majina na majina ya washambuliaji wanaotajwa huenda wakasajiliwa klabuni hapo kama mshambuliaji  SSC Napoli Gonzalo Higuain na Antoine  Griezmann wa Atletico Madrid...

VICTOR WANYAMA AFANAYA MAAMUZI MAGUMU NA KUWASHANGAZA VIONGOZI WA CLUB YA SOUTHAMPTONI.........................

Kiungo wa club ya southamptoni,anaetokea nchini kenya, Victor Wanyama , Afanya maamuzi mazito na kuwashangaza Viongozi wa club hiyo.
kiungo kutoka nchini kenya ,Victor wanyama ameugomea uongozi wa klabu hiyo ya southampton  katika suala la kusaini  mkataba mpya kwa kushinikiza kuondoka klabuni hapo.
Wanyama amefanya maamuzi hayo , huku ikifahamika aliyekua meneja wa the saint, Mauricio pochettino anahitaji kuona akikamilisha harakati za kumsajili wakati wa dirisha la usajili ili wawe wote Tttenham Hotspurs.
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu ya southampton ambayo ilimsajili akitokea celtic mwaka 2013 kwa ada ya pauni millioni 12.5.
Kutokana na hatua hiyo  uongozi wa The saint kwa sasa unasubiri ofa yoyote itakayomlenga kiungo huyo na tayari wameshaweka wazi thamani yake kwa kitaja kiasi cha pauni millionib25.
Klabu bigwa nchini England Leicester city , pia inatajwa kuwa katika mlolongo wa kutuma ofa St Marys, ili kuangalia uwezekano wa kumsajili wanyama.
Wanyama, anapigiwa upatu wa kusajiliwa huko king power stadium, ili kuwa sehemu ya mbadala wa kiungo kutoka nchini ufaransa NGolo kante ambaye amegoma kusaini mkataba  mpya...

MABIGWA WA LIGI KUU NCHINI WINGEREZA LEICESTER CITY , WAKUBALI KUMWACHIA MSHAMBULIAJI WAO MMOJA KWA CLUB YA NCHINI UJERUMANI....

Mabigwa wapya wa soka Nchini  England Leicester City Wakubali kumuachia Mshambuliaji Aliyewasababishia  Gharama kubwa za usajili Mwanzoni mwa msimu huu .
Mabigwa hao wa soka nchini England, wamekubali kumuuza  Mshambuliaji  wao kutoka nchini croatia , ambaye aliwagharimu kiasi kikubwa cha pesa katika usajili wake mwanzoni mwa msimu huu, Andrej kramaric.
Leicester city wametoa baraka za kuondoka kwa kramaric, baada ya kukamilisha  mazungumzo ya biashara na uongozi wa klabu ya Hffenheim ya nchini ujerumani.
Kramaric alisajiliwa na The foxes mwaka 2015, akitokea kwenye klabu ya HNK Rijeka ya nchini Croatia kwa ada ya uhamisho wa  pauni millioni 9.7, lakini mwezi januari alipelekwa kwa mkopo nchini ujherumani katika klabu ya hoffenheim.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameuzwa kwa bei ya hasara ya pauni milioni 8, na amekubali kusaini mkataba wa miaka minne na klabu ya hoffenheim.
Kramaric, alilazimika kuondoka king power stadium wakati wa dirisha dogo la usajili, kufuatia kushindwa kupata nafasi ya kucheza kila mwishoni mwa juma, na kwake kutokana na uwezo wa washambuliaji wengine  klabuni hapo.
Uongozi wa Hffenheim, umefikia maamuzi ya kumsajili  moja kwa moja Kramaric, baada ya kuridhishwa na uwezo wake kisoka ambao ulisaidia kuinusuru klabu hiyo isishuke daraja msimu wa 2015-16.

CHIDI BENZ AKIMBIA SOBER HOUSE BAADA YA KUKAA KWA SIKU 28 PEKE YAKE...........

Msanii wa kizazi kipya  Chid Benz anadaiwa kutoroka sober house baada ya kukaa kwa siku 28.
Rapa mkali wa Ilala Chid Benzi , alikua kwenye matibabu ya kupambana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya huko Bagamoyo.
taarifa mpya ni kwamba rapa huyo ametoroka katika jumba hilo baada ya kukaa kwa siku 28 pekee.
Akizungumza na Global Publishers meneja wa kituo hicho,Tumaini Majura, amedhibitisha kuondoka kwa chidi akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu.
''Ni siku 28 tu alikaa, lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida,,alisema Tumaini.
Aliongeza ''Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maan siku moja meneja wake [Babu Tale] alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondoka alingangania kuondoka nae.sisi pamoja na tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa,,
Pia Global walimtafuta chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.
Babu tale alipoulizwa kuhusu mwala hilo alisema'' sitaki kusikiliza wala kuzungumza lolote kuhusu Chid,muda ukifika nitaongea ila kwa sasa  niacheni  tu,, 

Jumatano, 25 Mei 2016

MANCHESTER UNITED WAPATA KIGUGUMIZI KUMTANGAZA JOSE MORINHO KAMA MENEJA MPYA WA MAN UNITED....

Klabu ya Manchester united  yapata kugugumizi kumtangaza  Jose Morinho rasmi kuwa kocha mpya wa club hiyo, kutokana na changamoto zinazowakabili kwa sasa.
Meneja mtarajiwa wa klabu ya Man utd, jose Morinho ameripotiwa kufikia makubaliano ya awali na uongozi wa klabu hiyo ya old Trafford ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Morinho alianza kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ya mjini  Manchster  mwishoni mwa juma lililopita, na amekubali kupokea mshahara wa pauni milioni 60 kwa mwaka .
Taarifa hizo zimeeleza kwamba huenda hii leo, pande hizo mbili zikasaini mkataba huo kabla ya kutangazwa kwa Jose Morinho kama meneja rasmi wa Man utd..

WEMA SEPETU AELEZA MACHUNGU ANAYOYAPATA KWA SABABU YA KUTOPATA MTOTO KWA KUPITIA MTANDAO WA INSTAGRAM

Msanii wa bongo movie nchini Wema Sepetu , ameandika ujumbe  kwa kupitia mtandao wa kijamii wa instagram juu ya maumivu  anayoyapata kutokana na kutokupata mtoto, 
Wema ni staa wa filamu aliyejizolea heshima za kutosha kutokana na umahiri wake katika kazi, lakini staa huyo analia na kukosa mtoto.
Wasanii wenzake na baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimpa faraja kila kukicha kuhusiana na swala hilo.
''iko siku na mimi mtaitwa mama,, ameandika kupitia ukurasa wake wa instagram akiambatanisha na picha aliyokumbatiana na mam yake.....

NEY WA MITEGO ATAJA LISTI YA WASANII WA KIKE WA BONGO MOVIE WANAO ONGOZA KUWACHAKAZA WASANII WA BONGO FLEVA WA KIUME WANAOCHIPUKIA..

Msanii wa kizazi kipya  Ney wa Mitego  amesema kuwa wasanii hawa wa bongo movie , Nisher, Wolper, na Shilole ndiyo wanawachakaza wasanii wa bongo fleva wa kiume ambao wanachipukia  na kufanya vizuri ,


Msanii huyo ambae anatamba sasa hivi na nyimbo yake inayoitwa saka hela, amekua ya desturi ya kutoa nyimbo zenye maneno ya kejeli kwa wasanii wenzake, moja ya nyimbo hizo ikiwa ni pamoja na shika adabu yako aliyoifanya chini ya producer T toucher, pamoja na nyimbo zingine nyingi..

Jumanne, 24 Mei 2016

PEP GUARDIOLA AANZA MIPANGO YA KUKISUKA UMPYA KIKOSI CHA MANCHESTER CITY......

kocha mpya wa club ya manchester city, yenye maskani yake katika jiji la manchester, nchini wingereza ameanza kazi ya kukitengeneza kikosi hiko, kwa kuanza harakati za usajili , taarifa zinasema muhispaniola huyo, ameanza mipango ya kumsajili kiungo  IIkay Gundogan.  
kiungo huyo kutoka nchini ujerumani  amekua  kivutio kikubwa cha meneja  huyo kutoka nchini  Hispania na alikaribia kusaini mkataba  na Man city mwezi  uliopita, lakini kikwazo kikawa majeraha ya goti yaliyomkabili.
Gundogan, bado ana mkataba na klabu ya Borussia  Dormund hadi mwaka 2017.
Ada yake ya uhamisho inatajwa kuwa Euro milioni 2 kama mgao wake ulioainishwa kwenye mkataba...

Ijumaa, 20 Mei 2016

ITAZAME NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA ALLY KIBA AJE.....

                                                 WATCH VIDEO         DOWNLOAD VIDEO

Jumanne, 17 Mei 2016

MKAZI WA KATA YA KAFUNZO WILAYANI SENGEREMA JIJINI MWANZA, JAMES MGAMBO [71] AMEUWAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA WATU WASIO JULIKANA..

Mtu mmoja ambae ni mkazi wa kata ya kafunzo wilayani serengeti ,James Mgambo  mwenye umri wa miaka 71 ameuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana ,ofisa Mtendaji wa kijiji cha Bilulumo ,said makelemo amesema mapanga mawili yaliyo aminika kutumika yalikutwa eneo la tukio,kwa mujibu wa Diwani wa kata ya kafunzo ,Dotto Bulunda ,mke wa mgambo  aliyetajwa kwa jina la nyangalo mansisa mwenye umri wa miaka 65 alijeruhiwa katika tukio hilo na amelazwa hospitali ya wilays ya sengerema , chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na polisi wamefika kwa ajili ya uchunguzi alisema Bulunda ofisa mtendaji wa kijiji cha  Bilulumo saidi makelemo alisema mapanga mawili yanayoaminika kutumika yalikutwa eneo la tukio mmoja wa majirani wa familia hiyo lameck kasabulilo alisema hawakusikia kelele za kuomba msaada .kwa mujibu wa msemaji wa familia hakimu Elisha, mazishi ya mgambo yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya ukoo yaliyopo kijijini hapo. mganga mkuu wa  hospitali teule wilaya ya serengerema Dk  mary jose alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa  chumba  cha kuhifadhi  maiti , huku hali ya  majeruhi ikiendelea vizuri  . mkuu wa wilaya sengerema , zainab Telack alisema tayari uchunguzi wa kina wa kuhusu  tukio hilo  umeanza na kuapa wahusika watasakwa na kutiwa mbaroni..

MSANII GIGY MONEY ATAKA KUWEKA REKODI KWA WANAUME WAZURI WOTE BONGO....

Msanii  wa bongo movie nchini tanzania Gigy Money atoa mpya baada ya kusema anataka kuweka rekodi ya kutembea na wanaume wazuri wote Bongo ..

Jumatano, 4 Mei 2016

BUNDUKI ZA KIVITA ZAKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TANGA ZILIZOTUMIKA KUFANYA UHALIFU......


Jeshi la polisi  mkoani Tanga  lakamata bunduki  za kivita  na sare  za kijeshi zilizotumika kufanya ualfu ,jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki tatu aina ya shtgun bastola  moja ,risasi 51 pamoja na mavazi ya jeshi la wananchi  ambazo zimetumika katika vitendo vya uhalifu kwa kupora fedha na mali mbalimbali kisha kkua mmoja kati ya wafanyabiashara wilayani kilindi , kamanda wa polisi  mkoani tanga kamishna msaidizi wa polisi  leonard paul amesema katika operesheni hiyo iliyofanyika katika kijiji cha kimamba  kilichopo kata ya  negero wilayani kilindi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kua kuwa kuna mtu anaejulikana kwa jina la tabu chabai anakiwanda cha kutengeneza silaha na ndipo walipokwenda kumpekua na kukuta silaha hizo.kamanda paul amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwakamatawaalifu, baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameelezea kuwa hatua hiyo imeanza kuwapa imani na jeshi hilo hasa baada ya matukio  mfululizo ya ujambazi yaliyotokea katika wilaya za kilindi na Tanga na kusababisha watu sita kuuwawa katika wilaya hizo kwa kupigwa risasi...

HILI NDILO KABURI ATAKALOPUMZISHWA MWANAMUZIKI PAPA WEMBA KABURI HILI LIMEJEGWA NJE KIDOGO YA MJI WA KINCHASA

Hili ndilo kaburi atakalozikwa nguli wa mziki barani afrika papa wemba ,kaburi hili liko pembeni kidogo ya mji wa kinchasa nchini kongo mwanamuziki huyo alikutwa na mauti nchini ivory coast alipokua akitumbuiza na kuanguka jukwaani na  kupoteza maisha  muda mfupi baadae....

HAYA NDIYO MANENO ALIYOYASEMA ROMA KUHUSU AINA YA MZIKI ANAO UFANYA.....

Mwanamuziki wa kizazi kipya roma mkatoliki  anasema ataanza kuimba  nyimbo za mapenzi au starehe pale utakapopatikana uongozi au utawala  utakaobadilisha taifa hili, najaribu kutafuta utawala au uongozi  utakaonifanya niimbe bata  nikianza kuimba bata  inamaana tumeshinda vita,ila kwa sasa naendelea kushindilia ili nibaki kuwa mwanaharakati hapa tanzania..

MWILI WA NGULI WA MUZIKI BARANI AFRIKA PAPA WEMBA KUPUMZISHWA LEO KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE...

Mazishi ya mwanamuziki nguli barani afrika papa wemba yanafanyika kijijini  kinchasa.umati  mkubwa wa watu umekusanyika  nje ya kanisa la Notre  Dame , kuhudhuria misa ,papa wemba anatarajiwa kuzikwa baadae leo jijini kinshasa..

CLUB YA CHELSEA YAZINDUA JEZI RASMI ITAKAYOTUMIKA MSIMU UJAO KATIKA MECHI ZAKE ZA NYUMBANI....

club ya chelsea imezindua jezi rasmi itakayokua inatumika katika mechi  zake za nyumbani kwa msimu ujao club hiyo amabyo imekua na msimu mbovu mwaka huu, imezindua jezi hiyo ikiwa tayari ni moja ya maandalizi kwa ajili ya msimo ujao wa ligi, club hiyo inatarajiwa kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya uefa barani ulaya kutokana na kukosa nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu nchini wingereza kwani mpaka sasa club hiyo inashika nafasi ya kumi ikiwa imebakiza michezo miwili peke yake..

USIKU WA ULAYA KUENDELEA LEO KATIKA HATUA YA NUSU FAINALI,MANCITY USO KWA USO NA REAL MADRID

Michuano ya club bigwa inatarajiwa kuendelea leo katika hatua ya nusu fainali, amabpo club ya real madrid itakabiliana na club ya manchester city ambayo imesafiri mpaka nchi spain katika jiji la madrid kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani wao katika michuano hiyo, katika mechi hiyo nyota wa real madrid cristiano ronaldo pamoja na mwenzake james wanatarajiwa kurudi katika mechi hiyo baada ya kuikosa mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa ETHAD jijini manchester...

CLUB YA LIVERPOOL YAJENGA UWANJA UTAKAO KUA WANNE KWA UKUBWA NCHINI WINGEREZA


uwanja wa club ya liver  pool unatarajiwa kuwa uwanja wa nne kwa ukubwa kati ya viwanja vya timu zinazoshiriki ligi kuu nchini wingereza uwanja huo  kwa sasa unaojegwa sasa ukikamilika unatarajiwa kuwa uwanja wenye uwezo wa kubeba mashabiki wengi zaidi tofauti na uwanja wanaoutumia kwa sasa.

RONALDO ASILIMIA MIA MOJA FIT TAYARI KUWAKABILI MANCHESTER CITY KATIKA MECHI YA NUSU FAINALI YA CLUB BIGWA BARANI ULAYA ,

Mshambuliaji wa club ya real madrid cristiano ronaldo ameruhusiwa rasmi na madaktari wa club hiyo kucheza mechi ya leo kati ya real madrid na manchestar city ,awali mshambuliaji huyo alikosa mechi ya kwanza iliyopigwa katika dimba la ETHAD STADIUM jijini manchester , na mechi hiyo kuisha kwa sare ya bila kufungana.mechi hiyo ya marudiano inachezwa leo katika dimba la santiago bernabeu nchini spain na itachezwa majira ya  saa 23:45 kwa saa za afrika ya mashariki..

VIJANA WA DIEGO PABLO SIMEONE ,ATLETICO MADRID HATIMAE WAFANIKIWA KUTINGA HATUA YA FAINALI KATIKA MICHUANO YA CLUB BIGWA BARANI ULAYA, UEFA CHAMPIONS LEAGUE

hatimae club ya atletico madrid yafanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kupata goli la ugenini lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa club hiyo antonio creizman, baada ya bayern kupata goli la kuongoza na mpaka mwisho wa mechi hiyo bayern 2- 1 atletico na matokeo ya jumla kua ni bayern 2-2 atletico madrid..

Jumanne, 3 Mei 2016

USIKU WA ULAYA KUENDELEA LEO, BAYERN MUNICH USO KWA USO NA ATLETICO MADRID KATIKA DIMBA LA ALIANCE ARENA NCHINI UJERUMANI.

nusu fainali ya michuano ya club bigwa barani ulaya kuendelea siku ya leo ambapo club ya atletico madrid itavaana na bayern munich katika dimba la aliance arena nchini ujerumani mechi ya kwanza club ya atletico madrid ilishinda goli moja kwa sifuri hivyo club ya bayern munich inakazi ya kuhakikisha inapindua matokeo hayo ili kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali katika katika michuano hiyo ya uefa champions league mechi hiyo itachezwa  23:45 kwa saa za afrika mashariki...

HATIMAE NDOTO YAKAMILIKA LEICESTER CITY, THE FOXES MABIGWA WAPYA LIGI KUU NCHINI WINGEREZA 2015,2016....

club ya leicester  city wametangazwa rasmi kua mabigwa wapya  wa EPL mwaka 2015,2016 baada ya jana club ya tothamhospurs kulazimishwa sare ya goli 2-2 na chelsea katika uwanja wa stanford bridger  amabpo ,Eden hazard ndiye mchezaji aliye wanyima ubigwa spurs baada ya kusawazisha goli dakika ya 85 na matokeo kua mbili,mbili ,club ya leicester city kutwaa ubigwa huo wa epl ni historia pekee kwa club hiyo na pia kwa kocha wao claudio raniery , kwani taji hilo la epl ni taji kubwa kabisa kwa kocha huyo kuwahi kulitwaa katika kazi yake ya ukocha......

Alhamisi, 28 Aprili 2016

TAIFA STARS KUCHUANA NA HARAMBEE STARS KATIKA MECHI YA KIRAFIKI IKIWA NI MOJA YA MAANDALIZI YA MICHUANO YA KUWANIA KUFUZU KWA FAINALI ZA MATAIFA AFRIKA MWEZI JUNI.

Timu ya taifa  Tifa stars  inatarajiwa kucheza  mechi ya kirafiki dhidi ya timu  ya taifa ya kenya harambee stars, mchezo huo utakua  ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote  mbili kujiandaa na  michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya afrika mwezi juni 2016 ambapo  Taifa stars itacheza  dhidi ya misri juni 04 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini  Dar es salam  TFF kwa kushirikiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi juni , kikosi cha  Taifa stars kinachonolewa na kocha mkuu charles Boniface  M kwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi mei mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya vodacom [VPL] kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili misri mwezi juni  2016 .......Chanzo  BBC...

ATLETICO MADRID YAJIWEKA NAFASI NZURI KUTINGA FAINALI YA MICHUANO YA CLUB BIGWA BARANI ULAYA BAADA YA KUPATA USHINDI WA GOLI MOJA KWA BILA DHIDI YA BAYERN MUNICH .


club ya Atletico Madrid yenye maskani yake nchini spain imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya club ya bayern Munich ya nchini ujerumani mechi  hiyo ni ya pili kuchezwa katika hatua ya nusu fainali  ya michuano ya club bigwa barani ulaya ambapo mechi ya kwanza  kwanza ilikua ni kati ya Real Madrid  na Manchester  City ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kutokufungana, mechi za marudiano zitachezwa wiki ijayo ambapo atletico  madrid watasafiri mpaka nhini Ujerumani kwa ajili ya kuwakabili bayern munich mchezo utakaopigwa katika uwanja wa alliance arena ,huku club ya manchester city wao watalazimika kusafiri mpaka nchini hispania  katika jiji la madrid ambapo watakabiliana na real madrid mchezo huo utapigwa katiaka uwanja wa santiago bernabeu.