C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Alhamisi, 16 Juni 2016

MUME AMUUA MKEWE KWA KUMNYONGA KWA KANGA KISA WIVU WA MAPENZI......

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rehema Tumbo amenyongwa na mumewe Raphael kazembe tena kwa kutumia khanga mkoani shinyanga kisa kikuu kikiwa ni wivu wa mapenzi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga Graiftoni mushi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na inadaiwa kuwa mwanamke huyo alichelewa kurudi na alipomgongea mumewe chumbani wanakolala hakumfungulia ndipo mwanaume huyo alipoamua kumfuata na kuanza kumpiga na kumnyonga hatimae kumsababishia mauti.
Mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio hili na mpaka sasa polisi wanaendelea na juhudi za kumsaka kokote aliko,mwenyekiti wa mtaa huo bwana Edward Mihayo anasema taarifa zilimfikia kutoka kwa wanamtaa baada ya kushuhudia maiti ya rehema ikiwa imenyongwa kwa kanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni