C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Alhamisi, 26 Mei 2016

VICTOR WANYAMA AFANAYA MAAMUZI MAGUMU NA KUWASHANGAZA VIONGOZI WA CLUB YA SOUTHAMPTONI.........................

Kiungo wa club ya southamptoni,anaetokea nchini kenya, Victor Wanyama , Afanya maamuzi mazito na kuwashangaza Viongozi wa club hiyo.
kiungo kutoka nchini kenya ,Victor wanyama ameugomea uongozi wa klabu hiyo ya southampton  katika suala la kusaini  mkataba mpya kwa kushinikiza kuondoka klabuni hapo.
Wanyama amefanya maamuzi hayo , huku ikifahamika aliyekua meneja wa the saint, Mauricio pochettino anahitaji kuona akikamilisha harakati za kumsajili wakati wa dirisha la usajili ili wawe wote Tttenham Hotspurs.
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu ya southampton ambayo ilimsajili akitokea celtic mwaka 2013 kwa ada ya pauni millioni 12.5.
Kutokana na hatua hiyo  uongozi wa The saint kwa sasa unasubiri ofa yoyote itakayomlenga kiungo huyo na tayari wameshaweka wazi thamani yake kwa kitaja kiasi cha pauni millionib25.
Klabu bigwa nchini England Leicester city , pia inatajwa kuwa katika mlolongo wa kutuma ofa St Marys, ili kuangalia uwezekano wa kumsajili wanyama.
Wanyama, anapigiwa upatu wa kusajiliwa huko king power stadium, ili kuwa sehemu ya mbadala wa kiungo kutoka nchini ufaransa NGolo kante ambaye amegoma kusaini mkataba  mpya...

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni