Jeshi la polisi mkoani Tanga lakamata bunduki za kivita na sare za kijeshi zilizotumika kufanya ualfu ,jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki tatu aina ya shtgun bastola moja ,risasi 51 pamoja na mavazi ya jeshi la wananchi ambazo zimetumika katika vitendo vya uhalifu kwa kupora fedha na mali mbalimbali kisha kkua mmoja kati ya wafanyabiashara wilayani kilindi , kamanda wa polisi mkoani tanga kamishna msaidizi wa polisi leonard paul amesema katika operesheni hiyo iliyofanyika katika kijiji cha kimamba kilichopo kata ya negero wilayani kilindi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kua kuwa kuna mtu anaejulikana kwa jina la tabu chabai anakiwanda cha kutengeneza silaha na ndipo walipokwenda kumpekua na kukuta silaha hizo.kamanda paul amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwakamatawaalifu, baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameelezea kuwa hatua hiyo imeanza kuwapa imani na jeshi hilo hasa baada ya matukio mfululizo ya ujambazi yaliyotokea katika wilaya za kilindi na Tanga na kusababisha watu sita kuuwawa katika wilaya hizo kwa kupigwa risasi... |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni