![]() | |
Meneja mpya wa klabu ya chelsea Antonio Conte Achafua Hali ya Hewa Stamford Brigder, baathi ya wachezaji hawajui Hatma Zao, |
Wakala wa mshambuliaji huyo aliyesajiliwa huko Stamford Bridger mwezi januari mwaka 2016, Gilmar Veloz amesema mpaka sasa wanasubiri maamuzi ya Conte ambaye yupo na kikosi cha timu ya taifa ya italia kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Euro 2016.
veloz, amesema tumaini lake kubwa kwa mshambuliaji huyo lipo mikononi mwa meneja huyo kutoka Italia, kutokana na kuamini bado kuna uwezekano wa pato kuendelea kubaki klabuni hapo.
Amesema anatambua Antonio conte atahitaji kuanza na mipango ya kuwatumia wachezaji atakao wasajili na wale watakaobaki kikosini, hivyo anaamini pato ni miongoni mwa watakaosubiri kauli ya mwisho ya mwitaliano huyo.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa chelsea wameshajihakikishia nafasi ya kuendelea kubaki klabuni hapo, huku wengine wakitambua fika hawana nafasi ya kucheza soka ndani ya club hiyo ya chelsea.
Mshambuliaji kutoka nchini hispsnia Diego costa anamatumaini makubwa ya kuendelea kusalia kwenye club hiyo, licha kuhusishwa na taarifa za kutakiwa na club yake ya zamani ya Atletico Madrid,huku mshambuliaji kinda Betrand Traore akiwa na matumaini kama hayo kufuatia uwezo wa kufunga mabao manne aliouonyesha wakati wa msimu wa 2015-16.
Mshambuliaji kutoka nchini Colombia, aliyekua akicheza kwa mkopo klabuni hapo Radamel Falcao tayari imeshafahamika anaondoka na kurejea katika klabu yake ya AS monaco ya Ufaransa huku kukiwa na mashaka kwa mshambuliaji Lic Remy.
Pia kumekua na majina na majina ya washambuliaji wanaotajwa huenda wakasajiliwa klabuni hapo kama mshambuliaji SSC Napoli Gonzalo Higuain na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni