![]() | |
Sarakasi za usajili wa kiungo kutoka ufaransa [PAUL POGBA]hatma ya uhamisho wa mchezaji huyo kujulikana ndani ya saa 48. |
Man united wanatarajia kukamilisha dili hilo kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya dunia, ambayo kwa sasa inashikwa na mshambuliaji kutoka Nchini wales na klabu ya Real madrid Gareth Bale.
Mashetani hao wekundu tayari wameshawasilisha ofa ya pauni milioni 100, huko Juventus stadium na baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa uongozi wa mabigwa wa soka nchini Italia Juventus umeshakubali.
Jambo lingine ambalo linaonyesha dalili za dili la wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda likakamilishwa ndani ya saa 48 zijazo ni mazungumzo ya uhamisho huo kati ya wakala wa Pogba Mino Raiola, na Mkurugenzi wa club hiyo ya Juventus Giusppe Beppe Moratta.
Mwanzo wawili hao walikua wakipingana kuhusu swala la uhamisho wa mchezaji huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni