![]() | |
Msanii wa kizazi kipya Chid Benz anadaiwa kutoroka sober house baada ya kukaa kwa siku 28. |
taarifa mpya ni kwamba rapa huyo ametoroka katika jumba hilo baada ya kukaa kwa siku 28 pekee.
Akizungumza na Global Publishers meneja wa kituo hicho,Tumaini Majura, amedhibitisha kuondoka kwa chidi akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu.
''Ni siku 28 tu alikaa, lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida,,alisema Tumaini.
Aliongeza ''Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maan siku moja meneja wake [Babu Tale] alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondoka alingangania kuondoka nae.sisi pamoja na tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa,,
Pia Global walimtafuta chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.
Babu tale alipoulizwa kuhusu mwala hilo alisema'' sitaki kusikiliza wala kuzungumza lolote kuhusu Chid,muda ukifika nitaongea ila kwa sasa niacheni tu,,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni