C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Alhamisi, 2 Juni 2016

MSANII RICH MAVOCO ASAINI RASMI MKATABA WA KUFANYA KAZI CHINI YA KAMPUNI YA WCB...............

Msanii wa mziki wa kizazi kipya rich mavoko asaini rasmi katika kampuni ya WCB inayomilikiwa na mwanamuziki Dimond Platnum.
Msanii huyo wa kizazi kipya ambae ni mkogwe katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya hapa nchini, amefikia uamuzi wa kusaini katika lebo hiyo ya wasafi baada ya kuridhishwa  na uendeshwaji wa kampuni hiyo iliyochini ya msanii mwenzake Dimond platnum,
Kampuni hiyo ya WCB kabla ya kumsainisha rich mavoco ilikua tayari imeshawasainisha wasanii wengine wawili wanao chipukia ambao ni Harmonize ambae tayari ananyimbo mbili zinazofanya vizuri kwa sasa nyimbo hizo ni  Aiyola,na Bado, huku mwenzake  Raymond akiwa na nyimbo mbili pia ya kwanza inaitwa huku kwetu, na ya pili Natafuta kick.
Mmiliki wa kampuni hiyo ya WCB aliandika haya katika akaunti yake ya facebok huku akiambatanisha na picha hii "welcome rich mavoco  let us take bongo fleva to the world,, aliandika dimond platnum.
Kusainiwa kwa msanii huyo rich mavoco katika lebo hiyo  anakua ndiye msanii wa kwanza mkogwe kusainiwa na lebo hiyo ya WCB..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni