![]() | ||
Mwanasiasa wa nchini marekani Donald Trump amesema mauaji ya watu 50 katika baa jana inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya marekani. |
upande wa bi clinton wakiton ambae ni mpinzani wa Donald trump katika kuwania kiti cha uraisi nchini marekani ,wametoa pole kwa waathirika wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Wakati huo,huo shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi wa jinsia moja alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.
Baba Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanae kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaoendeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani sitora yusufiy, amemweleza Mateen kama mtu aliyekuwa na tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni