C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Jumatano, 13 Julai 2016

THIERY HENRY AAMUA KUACHANA NA KAZI YA UKOCHA KATIKA CLUB YA ARSENAL.......................................

Gazeti la The sun linaripoti kuwa Thiery Henry ameachanana kazi ya ukocha wa muda wa timu ya vijana ya Arsenal baada ya kupishana kauli na meneja Arsener Wenger kufuatia kazi yake ya uchambuzi wa masuala ya soka kwenye Television.
Thiery Henry alikua anafanya kazi kwa part time na Arsenal ,kama kocha wa vijana chini ya umri wa miaka 18,alipata leseni ya UEFA  wakati huohuo akiwa ni mchambuzi wa kituo cha Television cha Sky sport, Henry aliomba kupewa mkataba wa kufanya kazi na Arsenal kwa msimu unaokuja kwa malipo kidogo, lakini boss wake Arsenel wenger alimpa mashsrti ya kufanya kazi hiyo kwa kumwambia kama anataka kazi hiyo basi aachane na kazi ya sky sports na kama anataka kazi Sky sport basi aachane na Arsenal.
Maamuzi aliyofanya Henry ambae ni gwiji wa soka wa zamani wa club hiyo yenye maskani yake katika jiji la London nchini wingereza, ameamua kuacha kazi katika Club hiyo na kubaki kuwa mchambuzi katika kituo cha Television cha Sky sport.
Maamuzi hayo yaliyofanywa na Gwiji huyo yamewafurahisha baadhi ya viongozi wa club hiyo ya Arsenal..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni