![]() | |
Mabigwa wapya wa soka Nchini England Leicester City Wakubali kumuachia Mshambuliaji Aliyewasababishia Gharama kubwa za usajili Mwanzoni mwa msimu huu . |
Leicester city wametoa baraka za kuondoka kwa kramaric, baada ya kukamilisha mazungumzo ya biashara na uongozi wa klabu ya Hffenheim ya nchini ujerumani.
Kramaric alisajiliwa na The foxes mwaka 2015, akitokea kwenye klabu ya HNK Rijeka ya nchini Croatia kwa ada ya uhamisho wa pauni millioni 9.7, lakini mwezi januari alipelekwa kwa mkopo nchini ujherumani katika klabu ya hoffenheim.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameuzwa kwa bei ya hasara ya pauni milioni 8, na amekubali kusaini mkataba wa miaka minne na klabu ya hoffenheim.
Kramaric, alilazimika kuondoka king power stadium wakati wa dirisha dogo la usajili, kufuatia kushindwa kupata nafasi ya kucheza kila mwishoni mwa juma, na kwake kutokana na uwezo wa washambuliaji wengine klabuni hapo.
Uongozi wa Hffenheim, umefikia maamuzi ya kumsajili moja kwa moja Kramaric, baada ya kuridhishwa na uwezo wake kisoka ambao ulisaidia kuinusuru klabu hiyo isishuke daraja msimu wa 2015-16.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni