![]() | |
Club ya Chelsea yenye maskani yake jijini london nchini Wingereza ipo katika hatua za mwisho kumsajili Mshambuliaji kutoka club ya Olmpic Marseille, Batshuayi kwa ada ya Euro million 33. |
Mchezaji huyo anatarajia kujiunga na mbelgiji mwenzake Eden hazard katika klabu hiyo ya chelsea katika msimu ujao.
Usajili huo ni wa kwanza kufanywa na club ya chelsea kwa msimu huu chini ya kocha mpya Antonio Conte, ikiwa ni moja ya harakati za kukiboresha kikosi cha club hiyo, kwani msimu uliopita haukua mzuri sana kwa club hiyo, iliyokua ikifundishwa na kocha jose morinho aliyetimuliwa klabuni hapo baada ya club hiyo kupata matokeo mabaya, kitu kilichopelekea kumaliza katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu nchini wingereza na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya klabui bigwa barani ulaya katika msimu ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni