![]() | |
Mamia ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherekea utamaduni katika mji wa Hull, uingereza. |
washiriki watapakwa rangi ya samawati jumamosi na kisha wapigwe picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa nampiga picha spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya sanaaa ya Ferens Art Gallery.
picha zitakazopigwa zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
Tunick, anayetoka New York, amewahi kufanya kazi kama hiyo kwingine.
Amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi sydney opera House, place des Art mjini Montrel, Mexico city na mjini Munich nchini Ujerumani.
Bw Tunick amesema kazi zake'' hugusia historia ndefu ya sanaaa ya utupu''
''Mavazi ni sanaa ya mtu mwingine''anasema.
Fashion ni sanaa. kwa kuondoa hilo[ mavazi] nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi wake''
Watu karibu 2000 wamejiandikisha kupigwa picha tangu wazo hilo litangazwe mwezi machi.
Baraza la mji wa Hull limesema baadhi ya barabara zitafungwa wakati wa shuhuli hiyo jumamosi asubuhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni