Mtu mmoja ambae ni mkazi wa kata ya kafunzo wilayani serengeti ,James Mgambo mwenye umri wa miaka 71 ameuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana ,ofisa Mtendaji wa kijiji cha Bilulumo ,said makelemo amesema mapanga mawili yaliyo aminika kutumika yalikutwa eneo la tukio,kwa mujibu wa Diwani wa kata ya kafunzo ,Dotto Bulunda ,mke wa mgambo aliyetajwa kwa jina la nyangalo mansisa mwenye umri wa miaka 65 alijeruhiwa katika tukio hilo na amelazwa hospitali ya wilays ya sengerema , chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na polisi wamefika kwa ajili ya uchunguzi alisema Bulunda ofisa mtendaji wa kijiji cha Bilulumo saidi makelemo alisema mapanga mawili yanayoaminika kutumika yalikutwa eneo la tukio mmoja wa majirani wa familia hiyo lameck kasabulilo alisema hawakusikia kelele za kuomba msaada .kwa mujibu wa msemaji wa familia hakimu Elisha, mazishi ya mgambo yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya ukoo yaliyopo kijijini hapo. mganga mkuu wa hospitali teule wilaya ya serengerema Dk mary jose alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti , huku hali ya majeruhi ikiendelea vizuri . mkuu wa wilaya sengerema , zainab Telack alisema tayari uchunguzi wa kina wa kuhusu tukio hilo umeanza na kuapa wahusika watasakwa na kutiwa mbaroni.. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni