 |
Mama wa Cristiano Ronaldo Dolores Aveiro amjia juu Dimitri payet,kufuatia rafu mbaya aliyomchezea mwanae katika fainali ya EURO 2016 Nchini Ufaransa. |
|
Malalamiko hayo yametolewa na mama mzazi wa cristiano Ronaldo,baada ya mwanae kuumia katika fainali ya kombe la michuano ya mabara ya ulaya UEFA EURO, ambapo katika mchezo huo wa fainali uliwakutanisha Timu ya taifa ya ureno dhidi ya Ufaransa waliokua wenyeji wa michuaano hiyo, ambapo katika kipindi cha kwanza mchezaji huyo aliumia baada ya kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa ufaransa Dimitri payet hali iliyopelekea mchezaji huyo kushindwa kuendelea na mchezo,huyo na kutolewa nje ya uwanja huku akitokwa machozi, hali iliyopelekea mama mzazi wa mchezaji huyo kuja juu na kudai kua mchezaji huyo wa ufaransa Dimitri Payet alikusudia kumchezea mwanae rafu hiyo kwa kuandia katika ukurasa wake katika mtandao wa twiter ''to play football is to kick a ball and not to kick the legs,,aliandika mama huyo.
Hata hivyo mechi hiyo iliisha kwa timu ya Taifa ya Ureno kufanikiwa kutwaa ubigwa wa michuano hiyo kwa kufanikiwa kuifunga Ufaransa goli moja kwa sifuri goli lililofugwa na mchezaji Heder katika dakika 30 za nyongeza baada ya kukamilika dakika 90 za kawaida bila mshindi kupatikana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni