C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

CLUB YA ARSENAL YAINGILIWA NA MAHASIMU WAO KATIKA DILI LA USAJILI...............

Washika bunduki wa kaskazini mwa jiji la London [ARSENAL] wamewasilisha maombi kwenye klabu ya Valencia na West Brom, wakitaka kuwa sajili shrodran mustafi na jonny Evans.
Arsenal wamewasilisha maombi hayo, lakini hawajaweka mezani dau kwa wachezaji hao wawili.
Huenda the Gunners wakapata upinzani mkali kutokakwa chelsea ambao wameonyesha nia ya kumsajili Mustaki ambaye aliwahi kuitumikia Klabu  ya Everton.
Mkataba wa Beki huyo kutoka nchini ujerumani unaonyesha kuwa  kama kuna klabu ikitaka kumsajili inatakiwa kutoa kiasi cha paundi milioni 41, lakini Valencia wamejishusha na kuwa tayari kupokea hadi pauni million 25.
Arsenal wanahitaji kuongeza beki mpya baaada ya nahodha wao per mertasecker  kusumbuliwa na majeraha amabayo huenda yakamweka nje hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Beki huyo wa ujerumani alipata majeraha hayo wakati wa mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya RC lens, ambapo  ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni