Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania muheshimiwa John pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji [TIC] juliet kairuki , uteuzi wake umetenguliwa kwa sababu ya kutochukua mshahara wake tangu mwaka 2013, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na katibu mkuu wa Biashara na uwekezaji ,prof Adolf Mkenda ,imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya raisi Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa mwaka 2013 hatua ambayo Rais amezua maswali mengi Aidha taarifa hiyo iliyosainiwa na katibu mkuu huyo imeongeza kuwa endapo BI kairuki atakua tayari kuendelea kufanaya kazi nyingine huku mchakato wa kumpata mkurugenzi mpya umeanza mara moja . kwa mujibu wa prof Mkenda bw clifford katondo tandali atakaimu nafasi ya mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho cha uwekezaji nchini TIC. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni