C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Alhamisi, 28 Aprili 2016

TAIFA STARS KUCHUANA NA HARAMBEE STARS KATIKA MECHI YA KIRAFIKI IKIWA NI MOJA YA MAANDALIZI YA MICHUANO YA KUWANIA KUFUZU KWA FAINALI ZA MATAIFA AFRIKA MWEZI JUNI.

Timu ya taifa  Tifa stars  inatarajiwa kucheza  mechi ya kirafiki dhidi ya timu  ya taifa ya kenya harambee stars, mchezo huo utakua  ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote  mbili kujiandaa na  michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya afrika mwezi juni 2016 ambapo  Taifa stars itacheza  dhidi ya misri juni 04 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini  Dar es salam  TFF kwa kushirikiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi juni , kikosi cha  Taifa stars kinachonolewa na kocha mkuu charles Boniface  M kwasa kinatarajiwa kuingia kambini mwezi mei mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya vodacom [VPL] kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili misri mwezi juni  2016 .......Chanzo  BBC...

ATLETICO MADRID YAJIWEKA NAFASI NZURI KUTINGA FAINALI YA MICHUANO YA CLUB BIGWA BARANI ULAYA BAADA YA KUPATA USHINDI WA GOLI MOJA KWA BILA DHIDI YA BAYERN MUNICH .


club ya Atletico Madrid yenye maskani yake nchini spain imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya club ya bayern Munich ya nchini ujerumani mechi  hiyo ni ya pili kuchezwa katika hatua ya nusu fainali  ya michuano ya club bigwa barani ulaya ambapo mechi ya kwanza  kwanza ilikua ni kati ya Real Madrid  na Manchester  City ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kutokufungana, mechi za marudiano zitachezwa wiki ijayo ambapo atletico  madrid watasafiri mpaka nhini Ujerumani kwa ajili ya kuwakabili bayern munich mchezo utakaopigwa katika uwanja wa alliance arena ,huku club ya manchester city wao watalazimika kusafiri mpaka nchini hispania  katika jiji la madrid ambapo watakabiliana na real madrid mchezo huo utapigwa katiaka uwanja wa santiago bernabeu.

MSANII KALA JEREMIAH AMESEMA HAONI SABABU YA KUPENYA KIMATAIFA KWANI HATA SOKO LA NDANI BADO HAJALIMALIZA

Msanii wa kizazi kipya kala Jeremiah  ameibuka na kusema kwa wakati huu haoni sababu ya yeye kuangaaika  kupenya kimataifa kwani bado hata soko la ndani hajalimaliza,msanii huyo kipaji chake kilianza kungaa katika mashindano ya kumtafuta mwanamuziki mwenye kipaji  bongo star search [BSS] ambapo kuanzia hapo ndicho nyota ya msanii huyo  ilipoanza kungaa na kufanya vizuri katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya hapa nchini..

MBUNGE WA KIGOMA MJINI ZITTO KABWE AIBUKA NA KUSEMA CCM NI ILE, ILE.......

Mbunge wa wa kigoma mjini kupitia chama cha  ACT  wazalendo  Zitto Kabwe ameibuka na kusema chama cha mapinduzi CCM ni kile kile  siku  zote  zitto kabwe amesema  hayo baada ya kusoma vitabu vya bajeti  ya mwaka huu na kusema bajeti hiyo ni ya kulipa deni la taifa, kwa mujibu wa zitto kabwe  amedai kuwa serikali inatarajia kukusanya shilingi trillioni 17 kwa mwaka na kusema  zaidi ya trilioni 8 zitakwenda kulipa deni la Taifa ambalo ni zaidi ya asilimia 50 ya bajeti na kusema ukichanganya na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni  nusu ya bajeti ni dhairi kwamba makusanyo ya serikali yataishia kilipa madeni na wafanyakazi , nimemaliza kusoma vitabu vya bajeti ya mwaka huu. kimsingi ni  Bajeti  ya kulipa deni la Taifa . wakati serikali inatarajia kukusanya shilingi trillion 17 mwaka huu shillingi trillioni 8 ikiwa ni asilimia 50 italipia deni la Taifa . ukiweka na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya bajeti ,ina maana makusanyo yote  ya serikali yatalipia madeni na mishahara . ndiyo maana serikali inaenda kukopa zaidi ya shilingi  trilioni 7 mwaka huu na kutegemea misaada ya wafadhili kwa shillingi trillion 5. ccm ni ileile  .....aliandika Zitto Kabwe.....

KITI CHA SPIKA WA BUNGE CHASEMA IPO HAJA YA KUFANYA MAREKEBISHO YA SHERIA NA KANUNI ZA BUNGE ILI KILA MMBUNGE APATE POSHO KULINGANA NA KAZI ALIYOIFANYA.

Kiti cha spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya sheria pamoja na kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya bungeni badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia  mahudhurio pekee ,aidha kimewataka wabunge kubadili na kuacha tabia ya kuchukua posho za vikao  vya bunge bila kuzitolea jasho

MWILI WA MWANAMUZIKI PAPA WEMBA WASAFIRISHWA KWENDA NCHINI CONGO KWA AJILI YA TARATIBU ZA MAZISHI.

Wanachi nchini congo wamejiandaa kuupokea mwili wa aliyekua nguli wa mziki barani afrika Papa Wemba ambae alifariki dunia nchini Ivory cost wakati akitumbuiza katika tamasha nchini huko baada ya kuanguaka gafla jukwaani wakati akiwa anatumbuiza na kuaga dunia muda mfupi baadae, mwiili wa mwanamuziki huyo unatarajiwa kuwasili nchini kongo nchi aliyozaliwa mwanamuziki huyo kwa ajili ya taratibu za mazishi, mwanamuziki huyo aliaga dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 66.

MAMA MARIA NYERERE MJANE WA RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE ATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI.

Mjane wa Rais wa kwanza  wa Tanzania  Baba  wa Taifa  Julius kambarage  nyerere pamoja na mwanae Mh. makongoro na msaidizi wake wametembelea  Daraja  jipya la julius  nyerere  kigamboni  Ameshukuru  Rais Magufuli  kwa kuamua  Daraja hilo liitwe  Daraja  la  Nerere kwa heshima ya baba wa taifa Mama maria amabe hakujali mvua kubwa iliyokua inanyesha alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa  na hayati mumewe imetimia .kwani amesema ni jambo amablo limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka muhasisi wa Taifa hili.

MLIMA KILIMANJARO WAPEWA TUZO YA KIVUTIO KINACHOONGOZA KULIKO VIVUTIO VYOTE BARANI AFRIKA MWAKA 2016

Mlima kilimanjaro uliopo  nchini Tanzania  umepewa  tuzo ya kivutio kinachooongoza kuliko vivutio vyote  Barani Afrika mwaka 2016 Taarifa hiyo imetolewa na Bodi ya Utalii Tanzania [TTB] mlima huo ulipewa tuzo hiyo  wakati wa utoaji wa tuzo za World Travel Awards African and Indian Ocean Gala Ceremony  sherehe hizo za utoaji wa tuzo hizo ulifanyikia visiwani Zanzibar.

MADEREVA WA MALORI KENYA WAGOMA, WATAKA MADEREVA WANAOTOKA TANZANIA WAONDOKE NCHINI HUMO..

Madereva wa malori nchini kenya wagoma wataka madereva wanaotoka Tanzania waondoke nchini humo madereva hao wameamua kuiandikia vizara husika barua inayowataka madereva wanao toka Tanzania kuondoka nchini humo  na kurudi  nchini kwao Tanzania.

RAIS JOHN MAGUFULI AMETENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA KITUO CHA UWEKEZAJI [TIC] JULIET KAIRUKI

Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania muheshimiwa John pombe Magufuli  ametengua  uteuzi wa mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji  [TIC] juliet  kairuki , uteuzi  wake umetenguliwa kwa sababu ya kutochukua mshahara wake  tangu mwaka 2013, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na katibu mkuu wa Biashara na uwekezaji ,prof  Adolf Mkenda ,imesema kuwa  hatua hiyo imekuja baada ya raisi  Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa  mwaka 2013 hatua ambayo Rais amezua maswali mengi  Aidha taarifa hiyo iliyosainiwa na katibu mkuu huyo imeongeza kuwa endapo BI kairuki atakua tayari kuendelea kufanaya kazi nyingine huku mchakato wa kumpata  mkurugenzi mpya umeanza mara moja . kwa mujibu wa prof Mkenda bw clifford katondo tandali atakaimu nafasi ya mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho cha uwekezaji nchini TIC.

Jumanne, 26 Aprili 2016

WACHEZAJI WA REAL MADRID WAKIWA NDANI YA NDEGE KATIKA SAFARI YA KUELEKEA KATIAKA JIJI LA MANCHESTER NCHINI WINGEREZA KUIKABILI MANCHESTER CITY.

Wachezaji wa club ya real madrid wakiwa katika ndege wakisafiri kuelekea nchini wingereza kwa ajili ya kuikabili club ya manchester city katika nusu fainali ya michuano ya club bigwa barani ulaya siku ya leo,madrid inayo ongozwa na kocha zinedine zidane imekua ikipata matokeo mazuri tangu kocha huyo alipoteuliwa kuchukua mikoba ya kocha Rafael benitez, aliyetimuliwa ndani ya club hiyo baada ya club kufanya vibaya...

JE LEISTER CITY ITAFANIKIWA KUPATA MATOKEO MBELE YA CLUB YA MANCHESTER UNITED HUKU IKIMKOSA MSHAMBULIAJI WAKE TEGEMEZI?

club ya leister city inayo ongoza msimamo wa ligi kuu nchini wingereza inakabililiwa na mchezo mgumu wikiend hii thidi ya manchester united baada ya kuibuka na ushindi wa magoli manne kwa bila dhidi ya swansea city wikiend iliyopita huku ikiwa haina mshambuliaji wake tegemezi vamie vady ambae pia ndie kinara wa ufungaji wa magoli kwenye ligi kuu nchini wingereza mpaka sas, hata hivyo wasiwasi kwa mashabiki wa club hiyo ni kua je club hiyo itaweza kupata matokeo wikiend hii pasipo kua na mshambuliaji wake vamie vady , mpaka sasa michezo ya ligi kuu nchini wingereza imebaki mitatu huku club hiyo ya leistercity wakiwa ndio vinara wanao ongoza ligi hiyo wakifuatiwa na club ya tothamhospurs wanaoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.

MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA LEO KATIKA NUSU FAINALI YA KWANZA KATIKA MICHUANO YA CLUB BIGWA BARANI ULAYA KATI YA MANCHESTER CITY VS REAL MADRID.

Nusu fainali ya  kwanza ya mashindano ya club bigwa barani ulaya kupigwa leo mashindano hayo yanayotambulika kwa jina la uefa champions league yatazikutanisha timu za manchester city na real madrid katika nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kupigwa katika jiji la manchester ambapo club ya real madrid wamesafir kutoka spain mpaka nchini wingereza kwa ajili ya pambano hilo linalotarajiwa kupigwa katika uwanaja wa ethad stadium wa manchester city ,timu hizo zilifanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya club ya manchester city kufanikiwa kuiondoa club ya paris saint jamein kwa jumla ya goli tatu kwa mbili, huku real madrid walifuzu hatua hiyo baada ya kuitoa timu ya wosburgy kutoka nchini ujerumani kwa jumla ya magoli matatu kwa mawili.mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 3:45 kwa saa za afrika ya mashariki...

Alhamisi, 21 Aprili 2016

TUCTA YAPINGA MPANGO WA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI KUKATA MISHAHARA KWA BAADHI YA WAKURUGENZI WA TAASISI ZA UMMA.

TUCTA imepinga  mpango  wa rais  Magufuli  kukata mishahara ya baadhi ya wakurugenzi wa Taasisi  za  umma kutoka milioni 40 mpaka milioni 15 , naibu katibu mkuu wa TUCTA  Hezron kaaya amesema uamuzi huo ni kinyume  na sheria  na utaligharimu Taifa iwapo wahusika wataamua kwenda mahakamani kupinga mishahara yao kupunguzwa......

PHILIPE SCHOLAR AMPA ONYO ANTONIO KONTE KABLA YA KUANZA KAZI YA KUINOA CLUB YA CHELSEA YENYE MASKANI YAKE JIJINI LONDON NCHINI WINGEREZA


kocha philip scholar amempa onyo kocha wa timu ya taifa ya italy ambae pia anatarajiwa msimu ujao kujiunga na club ya chelsea ya nchini england amabapo kocha  huyo ameshasaini mkataba wa miaka mitatu kwa ajili ya kuitumikia club hiyo kwa msimu ujao

Jumanne, 5 Aprili 2016

HII HAPA BARUA RASMI KUTOKA KWA RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MUHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI JUU YA KUFUTWA KWA SHEREHE ZA MUUNGANO....

Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania muheshimiwa John  Pombe  Magufuli  ametangaza rasmi kufuta sherehe za muungano amabazo hufanyika tarehe 26  april kila mwaka na kusema fedha zilizokua zitumike kuadhimisha siku hiyo zikatumike katika ujenzi wau panuz iwa barabara ya Air port jijini Mwanza.....

CLUB YA MANCHESTER UNITED YAFANIKIWA KUPUNGUZA TOFAUTI YA POINT KATI YAO NA MAHASUMU WAO CLUB YA MANCHESTER CITY NA KUBAKI TOFAUTI YA POINT MOJA....


Hii ndio tofauti ya point kati ya manchester  united na mancherster city baada ya club hiyo ya man united kushinda michezo mitatu mfululizo bila kupoteza ,ambapo wikiend iliyopita walifanikiwa kuichapa everton goli moja kwa bila  goli lililofugwa na antony martial na kufanikiwa kufikisha point 53  wakiwa katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi..

ANTONIO CONTE ATANGAZWA RASMI KUA KOCHA WA CLUB YA CHELSEA MSIMU UJAO,KWA KUSAINI MKATABA WA MIAKA MITATU

Hatimae  Antonio konte ametangaza kuwa kocha rasmi wa club ya chelsea yenye makazi yake jijini London nchini wingereza  kocha huyo alitangazwa rasmi  jana jumatatu kua kocha mpya wa club hiyo ya chelsea kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia club hiyo,kocha huyo anatarajiwa kujiunga na club hiyo msimu ujao, kwani kwa sasa kocha huyo yupo na timu ya Taifa ya Italy ambayo itashiriki michuano ya euro  2016 ......

Ijumaa, 1 Aprili 2016

RAPPER FAT JOE KUTOKA NCHINI MAREKANI AAMUA KUJIKITA ZAIDI KATIKA BIASHARA ,.....

Hatimae rapper fat joe kutoka nchini Marekani aamua kujikita katika biasha zaidi, kwa kujihusisha na biashara ya supermarkets akifanya mahojiano na kituo kimoja television nchini humo alisema kwangu haya ni maamuzi sahihi na pia nahisi huu ni wakati muafaka kwangu kufanya hiki ninachokifanaya kwa sasa,rapper huyo amekua kimya kwa  muda sasa baada ya kutamba kwa muda katika tasnia ya muziki akiwa na nyimbo kama vile make it rain aliyomshirikisha Lily wayne, na zinginezo............

TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAKUKURU YAWABURUZA WABUNGE WATATU MAHAKAMANI

Pichani ni Wabunge wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania,wa kwanza kutoka kushoto ni  Mh.victor mwambalaswa Mbunge wa lupa, wapili ni Mh saidi Murad Mbunge wa Mvomero ,na watatu ni Mh kangi lugola Mbunge wa Mwibara, wakiwa katika mahakama ya kisutu kujibu mashtaka yaulaji rushwa yanayo wakabili, wabunge hao walifikishwa kwenye mahakama hiyo na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU , kwa ajili ya kujibu mashtaka hayo yanayo wakabili, Wabunge hao wamekumbwa na kashfa hiyo wakiwa katika kamati za  kudumu za bunge...

HATIMAE EURA YASHUSHA RASMI BEI YA UMEME KUANZIA LEO TAREHE 1 -4-2016,IKIWA NI HATUA YA KUTIMIZA OMBI LA SHIRIKA LA UMEME NCHINI TANESCO

Baada ya shirika la umeme Tanzania TANESCO kutuma maombi ya kushushwa kwa bei za umeme ,hatimae EURA yatanga rasmi kushusha bei ya umeme kuanzia leo tarehe 1-4-2016 ,pamoja na garama zingine kama vile service chaji kwa baadhi ya wateja kulingana na matumizi ya mteja husika..

HIZI NDIZO REKODI ZA WAKALI WAWILI WA SOKA DUNIANI KUELEKEA PAMBANO LA ELCLASSICO SIKU YA KESHO TAREHE 2

Record kali za wakali  wawili wa soka duniani lionel messi  pamoja na cristiano ronaldo