C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Alhamisi, 26 Mei 2016

ANTONIO CONTE ACHAFUA HALI YA HEWA NDANI YA CLUB YA CHELSEA.............

Meneja mpya wa klabu ya chelsea Antonio Conte Achafua Hali ya  Hewa Stamford Brigder, baathi ya wachezaji hawajui Hatma Zao,
Majaaliwa ya mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Alexandre Pato ya kuendelea kucheza ndani ya kikosi cha chelsea, yapo mikononi mwa meneja mpya wa klabu hiyo Antonio Conte.
 Wakala wa mshambuliaji huyo aliyesajiliwa huko Stamford Bridger mwezi januari mwaka  2016, Gilmar Veloz amesema mpaka sasa wanasubiri maamuzi ya Conte ambaye yupo na kikosi cha timu ya taifa ya italia kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Euro 2016.
veloz, amesema tumaini lake kubwa kwa mshambuliaji huyo lipo mikononi mwa meneja huyo kutoka  Italia, kutokana na kuamini bado  kuna uwezekano wa pato kuendelea kubaki klabuni hapo.
Amesema anatambua Antonio conte atahitaji kuanza na mipango ya kuwatumia wachezaji atakao wasajili na wale watakaobaki  kikosini, hivyo anaamini pato ni miongoni mwa watakaosubiri kauli ya mwisho ya mwitaliano huyo.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa chelsea wameshajihakikishia nafasi ya kuendelea kubaki klabuni hapo, huku wengine wakitambua fika hawana nafasi ya kucheza soka ndani ya club hiyo ya chelsea.
Mshambuliaji kutoka nchini hispsnia Diego costa anamatumaini makubwa ya kuendelea kusalia kwenye club hiyo, licha kuhusishwa na taarifa za kutakiwa na club yake ya zamani ya Atletico Madrid,huku mshambuliaji kinda Betrand Traore akiwa na matumaini kama hayo kufuatia uwezo wa kufunga mabao manne aliouonyesha wakati wa msimu wa 2015-16.
Mshambuliaji kutoka nchini Colombia, aliyekua akicheza kwa mkopo klabuni hapo Radamel Falcao tayari imeshafahamika anaondoka na kurejea katika klabu yake ya AS monaco ya Ufaransa huku kukiwa na mashaka  kwa mshambuliaji Lic Remy.
Pia kumekua na majina na majina ya washambuliaji wanaotajwa huenda wakasajiliwa klabuni hapo kama mshambuliaji  SSC Napoli Gonzalo Higuain na Antoine  Griezmann wa Atletico Madrid...

VICTOR WANYAMA AFANAYA MAAMUZI MAGUMU NA KUWASHANGAZA VIONGOZI WA CLUB YA SOUTHAMPTONI.........................

Kiungo wa club ya southamptoni,anaetokea nchini kenya, Victor Wanyama , Afanya maamuzi mazito na kuwashangaza Viongozi wa club hiyo.
kiungo kutoka nchini kenya ,Victor wanyama ameugomea uongozi wa klabu hiyo ya southampton  katika suala la kusaini  mkataba mpya kwa kushinikiza kuondoka klabuni hapo.
Wanyama amefanya maamuzi hayo , huku ikifahamika aliyekua meneja wa the saint, Mauricio pochettino anahitaji kuona akikamilisha harakati za kumsajili wakati wa dirisha la usajili ili wawe wote Tttenham Hotspurs.
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu ya southampton ambayo ilimsajili akitokea celtic mwaka 2013 kwa ada ya pauni millioni 12.5.
Kutokana na hatua hiyo  uongozi wa The saint kwa sasa unasubiri ofa yoyote itakayomlenga kiungo huyo na tayari wameshaweka wazi thamani yake kwa kitaja kiasi cha pauni millionib25.
Klabu bigwa nchini England Leicester city , pia inatajwa kuwa katika mlolongo wa kutuma ofa St Marys, ili kuangalia uwezekano wa kumsajili wanyama.
Wanyama, anapigiwa upatu wa kusajiliwa huko king power stadium, ili kuwa sehemu ya mbadala wa kiungo kutoka nchini ufaransa NGolo kante ambaye amegoma kusaini mkataba  mpya...

MABIGWA WA LIGI KUU NCHINI WINGEREZA LEICESTER CITY , WAKUBALI KUMWACHIA MSHAMBULIAJI WAO MMOJA KWA CLUB YA NCHINI UJERUMANI....

Mabigwa wapya wa soka Nchini  England Leicester City Wakubali kumuachia Mshambuliaji Aliyewasababishia  Gharama kubwa za usajili Mwanzoni mwa msimu huu .
Mabigwa hao wa soka nchini England, wamekubali kumuuza  Mshambuliaji  wao kutoka nchini croatia , ambaye aliwagharimu kiasi kikubwa cha pesa katika usajili wake mwanzoni mwa msimu huu, Andrej kramaric.
Leicester city wametoa baraka za kuondoka kwa kramaric, baada ya kukamilisha  mazungumzo ya biashara na uongozi wa klabu ya Hffenheim ya nchini ujerumani.
Kramaric alisajiliwa na The foxes mwaka 2015, akitokea kwenye klabu ya HNK Rijeka ya nchini Croatia kwa ada ya uhamisho wa  pauni millioni 9.7, lakini mwezi januari alipelekwa kwa mkopo nchini ujherumani katika klabu ya hoffenheim.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameuzwa kwa bei ya hasara ya pauni milioni 8, na amekubali kusaini mkataba wa miaka minne na klabu ya hoffenheim.
Kramaric, alilazimika kuondoka king power stadium wakati wa dirisha dogo la usajili, kufuatia kushindwa kupata nafasi ya kucheza kila mwishoni mwa juma, na kwake kutokana na uwezo wa washambuliaji wengine  klabuni hapo.
Uongozi wa Hffenheim, umefikia maamuzi ya kumsajili  moja kwa moja Kramaric, baada ya kuridhishwa na uwezo wake kisoka ambao ulisaidia kuinusuru klabu hiyo isishuke daraja msimu wa 2015-16.

CHIDI BENZ AKIMBIA SOBER HOUSE BAADA YA KUKAA KWA SIKU 28 PEKE YAKE...........

Msanii wa kizazi kipya  Chid Benz anadaiwa kutoroka sober house baada ya kukaa kwa siku 28.
Rapa mkali wa Ilala Chid Benzi , alikua kwenye matibabu ya kupambana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya huko Bagamoyo.
taarifa mpya ni kwamba rapa huyo ametoroka katika jumba hilo baada ya kukaa kwa siku 28 pekee.
Akizungumza na Global Publishers meneja wa kituo hicho,Tumaini Majura, amedhibitisha kuondoka kwa chidi akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu.
''Ni siku 28 tu alikaa, lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida,,alisema Tumaini.
Aliongeza ''Nafikiri ni uamuzi wake binafsi maan siku moja meneja wake [Babu Tale] alikuja kumjulia hali, alipotaka kuondoka alingangania kuondoka nae.sisi pamoja na tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa,,
Pia Global walimtafuta chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.
Babu tale alipoulizwa kuhusu mwala hilo alisema'' sitaki kusikiliza wala kuzungumza lolote kuhusu Chid,muda ukifika nitaongea ila kwa sasa  niacheni  tu,, 

Jumatano, 25 Mei 2016

MANCHESTER UNITED WAPATA KIGUGUMIZI KUMTANGAZA JOSE MORINHO KAMA MENEJA MPYA WA MAN UNITED....

Klabu ya Manchester united  yapata kugugumizi kumtangaza  Jose Morinho rasmi kuwa kocha mpya wa club hiyo, kutokana na changamoto zinazowakabili kwa sasa.
Meneja mtarajiwa wa klabu ya Man utd, jose Morinho ameripotiwa kufikia makubaliano ya awali na uongozi wa klabu hiyo ya old Trafford ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Morinho alianza kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ya mjini  Manchster  mwishoni mwa juma lililopita, na amekubali kupokea mshahara wa pauni milioni 60 kwa mwaka .
Taarifa hizo zimeeleza kwamba huenda hii leo, pande hizo mbili zikasaini mkataba huo kabla ya kutangazwa kwa Jose Morinho kama meneja rasmi wa Man utd..

WEMA SEPETU AELEZA MACHUNGU ANAYOYAPATA KWA SABABU YA KUTOPATA MTOTO KWA KUPITIA MTANDAO WA INSTAGRAM

Msanii wa bongo movie nchini Wema Sepetu , ameandika ujumbe  kwa kupitia mtandao wa kijamii wa instagram juu ya maumivu  anayoyapata kutokana na kutokupata mtoto, 
Wema ni staa wa filamu aliyejizolea heshima za kutosha kutokana na umahiri wake katika kazi, lakini staa huyo analia na kukosa mtoto.
Wasanii wenzake na baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimpa faraja kila kukicha kuhusiana na swala hilo.
''iko siku na mimi mtaitwa mama,, ameandika kupitia ukurasa wake wa instagram akiambatanisha na picha aliyokumbatiana na mam yake.....

NEY WA MITEGO ATAJA LISTI YA WASANII WA KIKE WA BONGO MOVIE WANAO ONGOZA KUWACHAKAZA WASANII WA BONGO FLEVA WA KIUME WANAOCHIPUKIA..

Msanii wa kizazi kipya  Ney wa Mitego  amesema kuwa wasanii hawa wa bongo movie , Nisher, Wolper, na Shilole ndiyo wanawachakaza wasanii wa bongo fleva wa kiume ambao wanachipukia  na kufanya vizuri ,


Msanii huyo ambae anatamba sasa hivi na nyimbo yake inayoitwa saka hela, amekua ya desturi ya kutoa nyimbo zenye maneno ya kejeli kwa wasanii wenzake, moja ya nyimbo hizo ikiwa ni pamoja na shika adabu yako aliyoifanya chini ya producer T toucher, pamoja na nyimbo zingine nyingi..

Jumanne, 24 Mei 2016

PEP GUARDIOLA AANZA MIPANGO YA KUKISUKA UMPYA KIKOSI CHA MANCHESTER CITY......

kocha mpya wa club ya manchester city, yenye maskani yake katika jiji la manchester, nchini wingereza ameanza kazi ya kukitengeneza kikosi hiko, kwa kuanza harakati za usajili , taarifa zinasema muhispaniola huyo, ameanza mipango ya kumsajili kiungo  IIkay Gundogan.  
kiungo huyo kutoka nchini ujerumani  amekua  kivutio kikubwa cha meneja  huyo kutoka nchini  Hispania na alikaribia kusaini mkataba  na Man city mwezi  uliopita, lakini kikwazo kikawa majeraha ya goti yaliyomkabili.
Gundogan, bado ana mkataba na klabu ya Borussia  Dormund hadi mwaka 2017.
Ada yake ya uhamisho inatajwa kuwa Euro milioni 2 kama mgao wake ulioainishwa kwenye mkataba...

Ijumaa, 20 Mei 2016

ITAZAME NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA ALLY KIBA AJE.....

                                                 WATCH VIDEO         DOWNLOAD VIDEO

Jumanne, 17 Mei 2016

MKAZI WA KATA YA KAFUNZO WILAYANI SENGEREMA JIJINI MWANZA, JAMES MGAMBO [71] AMEUWAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA WATU WASIO JULIKANA..

Mtu mmoja ambae ni mkazi wa kata ya kafunzo wilayani serengeti ,James Mgambo  mwenye umri wa miaka 71 ameuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana ,ofisa Mtendaji wa kijiji cha Bilulumo ,said makelemo amesema mapanga mawili yaliyo aminika kutumika yalikutwa eneo la tukio,kwa mujibu wa Diwani wa kata ya kafunzo ,Dotto Bulunda ,mke wa mgambo  aliyetajwa kwa jina la nyangalo mansisa mwenye umri wa miaka 65 alijeruhiwa katika tukio hilo na amelazwa hospitali ya wilays ya sengerema , chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na polisi wamefika kwa ajili ya uchunguzi alisema Bulunda ofisa mtendaji wa kijiji cha  Bilulumo saidi makelemo alisema mapanga mawili yanayoaminika kutumika yalikutwa eneo la tukio mmoja wa majirani wa familia hiyo lameck kasabulilo alisema hawakusikia kelele za kuomba msaada .kwa mujibu wa msemaji wa familia hakimu Elisha, mazishi ya mgambo yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya ukoo yaliyopo kijijini hapo. mganga mkuu wa  hospitali teule wilaya ya serengerema Dk  mary jose alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa  chumba  cha kuhifadhi  maiti , huku hali ya  majeruhi ikiendelea vizuri  . mkuu wa wilaya sengerema , zainab Telack alisema tayari uchunguzi wa kina wa kuhusu  tukio hilo  umeanza na kuapa wahusika watasakwa na kutiwa mbaroni..

MSANII GIGY MONEY ATAKA KUWEKA REKODI KWA WANAUME WAZURI WOTE BONGO....

Msanii  wa bongo movie nchini tanzania Gigy Money atoa mpya baada ya kusema anataka kuweka rekodi ya kutembea na wanaume wazuri wote Bongo ..

Jumatano, 4 Mei 2016

BUNDUKI ZA KIVITA ZAKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TANGA ZILIZOTUMIKA KUFANYA UHALIFU......


Jeshi la polisi  mkoani Tanga  lakamata bunduki  za kivita  na sare  za kijeshi zilizotumika kufanya ualfu ,jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki tatu aina ya shtgun bastola  moja ,risasi 51 pamoja na mavazi ya jeshi la wananchi  ambazo zimetumika katika vitendo vya uhalifu kwa kupora fedha na mali mbalimbali kisha kkua mmoja kati ya wafanyabiashara wilayani kilindi , kamanda wa polisi  mkoani tanga kamishna msaidizi wa polisi  leonard paul amesema katika operesheni hiyo iliyofanyika katika kijiji cha kimamba  kilichopo kata ya  negero wilayani kilindi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kua kuwa kuna mtu anaejulikana kwa jina la tabu chabai anakiwanda cha kutengeneza silaha na ndipo walipokwenda kumpekua na kukuta silaha hizo.kamanda paul amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwakamatawaalifu, baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameelezea kuwa hatua hiyo imeanza kuwapa imani na jeshi hilo hasa baada ya matukio  mfululizo ya ujambazi yaliyotokea katika wilaya za kilindi na Tanga na kusababisha watu sita kuuwawa katika wilaya hizo kwa kupigwa risasi...

HILI NDILO KABURI ATAKALOPUMZISHWA MWANAMUZIKI PAPA WEMBA KABURI HILI LIMEJEGWA NJE KIDOGO YA MJI WA KINCHASA

Hili ndilo kaburi atakalozikwa nguli wa mziki barani afrika papa wemba ,kaburi hili liko pembeni kidogo ya mji wa kinchasa nchini kongo mwanamuziki huyo alikutwa na mauti nchini ivory coast alipokua akitumbuiza na kuanguka jukwaani na  kupoteza maisha  muda mfupi baadae....

HAYA NDIYO MANENO ALIYOYASEMA ROMA KUHUSU AINA YA MZIKI ANAO UFANYA.....

Mwanamuziki wa kizazi kipya roma mkatoliki  anasema ataanza kuimba  nyimbo za mapenzi au starehe pale utakapopatikana uongozi au utawala  utakaobadilisha taifa hili, najaribu kutafuta utawala au uongozi  utakaonifanya niimbe bata  nikianza kuimba bata  inamaana tumeshinda vita,ila kwa sasa naendelea kushindilia ili nibaki kuwa mwanaharakati hapa tanzania..

MWILI WA NGULI WA MUZIKI BARANI AFRIKA PAPA WEMBA KUPUMZISHWA LEO KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE...

Mazishi ya mwanamuziki nguli barani afrika papa wemba yanafanyika kijijini  kinchasa.umati  mkubwa wa watu umekusanyika  nje ya kanisa la Notre  Dame , kuhudhuria misa ,papa wemba anatarajiwa kuzikwa baadae leo jijini kinshasa..

CLUB YA CHELSEA YAZINDUA JEZI RASMI ITAKAYOTUMIKA MSIMU UJAO KATIKA MECHI ZAKE ZA NYUMBANI....

club ya chelsea imezindua jezi rasmi itakayokua inatumika katika mechi  zake za nyumbani kwa msimu ujao club hiyo amabyo imekua na msimu mbovu mwaka huu, imezindua jezi hiyo ikiwa tayari ni moja ya maandalizi kwa ajili ya msimo ujao wa ligi, club hiyo inatarajiwa kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya uefa barani ulaya kutokana na kukosa nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu nchini wingereza kwani mpaka sasa club hiyo inashika nafasi ya kumi ikiwa imebakiza michezo miwili peke yake..

USIKU WA ULAYA KUENDELEA LEO KATIKA HATUA YA NUSU FAINALI,MANCITY USO KWA USO NA REAL MADRID

Michuano ya club bigwa inatarajiwa kuendelea leo katika hatua ya nusu fainali, amabpo club ya real madrid itakabiliana na club ya manchester city ambayo imesafiri mpaka nchi spain katika jiji la madrid kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani wao katika michuano hiyo, katika mechi hiyo nyota wa real madrid cristiano ronaldo pamoja na mwenzake james wanatarajiwa kurudi katika mechi hiyo baada ya kuikosa mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa ETHAD jijini manchester...

CLUB YA LIVERPOOL YAJENGA UWANJA UTAKAO KUA WANNE KWA UKUBWA NCHINI WINGEREZA


uwanja wa club ya liver  pool unatarajiwa kuwa uwanja wa nne kwa ukubwa kati ya viwanja vya timu zinazoshiriki ligi kuu nchini wingereza uwanja huo  kwa sasa unaojegwa sasa ukikamilika unatarajiwa kuwa uwanja wenye uwezo wa kubeba mashabiki wengi zaidi tofauti na uwanja wanaoutumia kwa sasa.

RONALDO ASILIMIA MIA MOJA FIT TAYARI KUWAKABILI MANCHESTER CITY KATIKA MECHI YA NUSU FAINALI YA CLUB BIGWA BARANI ULAYA ,

Mshambuliaji wa club ya real madrid cristiano ronaldo ameruhusiwa rasmi na madaktari wa club hiyo kucheza mechi ya leo kati ya real madrid na manchestar city ,awali mshambuliaji huyo alikosa mechi ya kwanza iliyopigwa katika dimba la ETHAD STADIUM jijini manchester , na mechi hiyo kuisha kwa sare ya bila kufungana.mechi hiyo ya marudiano inachezwa leo katika dimba la santiago bernabeu nchini spain na itachezwa majira ya  saa 23:45 kwa saa za afrika ya mashariki..

VIJANA WA DIEGO PABLO SIMEONE ,ATLETICO MADRID HATIMAE WAFANIKIWA KUTINGA HATUA YA FAINALI KATIKA MICHUANO YA CLUB BIGWA BARANI ULAYA, UEFA CHAMPIONS LEAGUE

hatimae club ya atletico madrid yafanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kupata goli la ugenini lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa club hiyo antonio creizman, baada ya bayern kupata goli la kuongoza na mpaka mwisho wa mechi hiyo bayern 2- 1 atletico na matokeo ya jumla kua ni bayern 2-2 atletico madrid..

Jumanne, 3 Mei 2016

USIKU WA ULAYA KUENDELEA LEO, BAYERN MUNICH USO KWA USO NA ATLETICO MADRID KATIKA DIMBA LA ALIANCE ARENA NCHINI UJERUMANI.

nusu fainali ya michuano ya club bigwa barani ulaya kuendelea siku ya leo ambapo club ya atletico madrid itavaana na bayern munich katika dimba la aliance arena nchini ujerumani mechi ya kwanza club ya atletico madrid ilishinda goli moja kwa sifuri hivyo club ya bayern munich inakazi ya kuhakikisha inapindua matokeo hayo ili kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali katika katika michuano hiyo ya uefa champions league mechi hiyo itachezwa  23:45 kwa saa za afrika mashariki...

HATIMAE NDOTO YAKAMILIKA LEICESTER CITY, THE FOXES MABIGWA WAPYA LIGI KUU NCHINI WINGEREZA 2015,2016....

club ya leicester  city wametangazwa rasmi kua mabigwa wapya  wa EPL mwaka 2015,2016 baada ya jana club ya tothamhospurs kulazimishwa sare ya goli 2-2 na chelsea katika uwanja wa stanford bridger  amabpo ,Eden hazard ndiye mchezaji aliye wanyima ubigwa spurs baada ya kusawazisha goli dakika ya 85 na matokeo kua mbili,mbili ,club ya leicester city kutwaa ubigwa huo wa epl ni historia pekee kwa club hiyo na pia kwa kocha wao claudio raniery , kwani taji hilo la epl ni taji kubwa kabisa kwa kocha huyo kuwahi kulitwaa katika kazi yake ya ukocha......