C E O OF BMG

- Black generation media Group [ BMG]
- FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.
Alhamisi, 28 Julai 2016
KOFFIE OLOMIDE ATUPWA JELA MIEZI 18 MJINI KINSHASA NCHINI CONGO............
![]() | |
Mahakama mjini kinshasa imemuhukumu mwanamuziki Mkogwe Koffie Olomide kwenda jela miezi 18 kwa kosa la kumpiga mngenguaji wake kudhalilisha utu wa mwanamke. |
Msanii huyo ameanza kutumikia adhabu yake katika gereza moja nchini humo na wakati akiingia kwenye gereza hilo Koffie alisikika akisema siwapendi wanawake,
KLABU YA VILLARREAL YAKAMILISHA USAJILI WA MSHAMBULIAJI KUTOKA CHELSEA......................................
![]() | |
Klabu ya Villarreal ya nchini Hispania imedhibitisha kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Brazil ,Alexandre pato |
Taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya klabuhiyo ya El Madrigal zimeeleza kuwa pato amesaini mkataba wa miaka minne.
Hata hivyo haikuelezwa ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kama ada ya usajili wa mshambuliji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye aliwahi kutamab na klabu ya AC milani ya nchini italia kuanzia mwaka 2007-2012.
Klabu ya sevilla cf ya nchini Hispania nayo ilikua inahusishwa na kutaka kumsajili Pato.
HATMA YA SAKATA LA KIUNGO PAUL POGBA KUTUA OLD TRAFORD KUJULIKANA NDANI YA SAA 48 ZIJAZO............
![]() | |
Sarakasi za usajili wa kiungo kutoka ufaransa [PAUL POGBA]hatma ya uhamisho wa mchezaji huyo kujulikana ndani ya saa 48. |
Man united wanatarajia kukamilisha dili hilo kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya dunia, ambayo kwa sasa inashikwa na mshambuliaji kutoka Nchini wales na klabu ya Real madrid Gareth Bale.
Mashetani hao wekundu tayari wameshawasilisha ofa ya pauni milioni 100, huko Juventus stadium na baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa uongozi wa mabigwa wa soka nchini Italia Juventus umeshakubali.
Jambo lingine ambalo linaonyesha dalili za dili la wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda likakamilishwa ndani ya saa 48 zijazo ni mazungumzo ya uhamisho huo kati ya wakala wa Pogba Mino Raiola, na Mkurugenzi wa club hiyo ya Juventus Giusppe Beppe Moratta.
Mwanzo wawili hao walikua wakipingana kuhusu swala la uhamisho wa mchezaji huyo.
RAPA NAY WA MITEGO ADAI ATAWAMIS......
![]() | |
Rapa Nay wa mitego ambae amefungiwa kujihusisha na shuhuli za muziki na Baraza la sanaa nchini BaSATA, amefunguka na kudai kuwa atazimiss shuhuli alizokua anazifanya. |
Basata imemfungia rapa huyo kwa kipindi amabacho hakijajulikana, mpaka pale watakapojiridhisha kwamba amebadilika ikiwemo kujisajili kufanya shuhuli za sanaa nchini.
Jumatano, 13 Julai 2016
KLABU YA CHELSEA YAZINDUA RASMI JEZI ITAKAYOTUMIKA KATIKA MSIMU UJAO WA LIGI KWA MECHI ZA UGENINI...........
![]() | |
klabu ya chelsea yenye maskani yake jijini london nchini wingereza yazindua rasmi jezi itakayo tumika katika mechi zake za ugenini. |
MAMA WA CRISTIANO RONALDO AMJIA JUU MCHEZAJI WA UFARANSA DIMITRI PAYET......................................
![]() | |
Mama wa Cristiano Ronaldo Dolores Aveiro amjia juu Dimitri payet,kufuatia rafu mbaya aliyomchezea mwanae katika fainali ya EURO 2016 Nchini Ufaransa. |
Hata hivyo mechi hiyo iliisha kwa timu ya Taifa ya Ureno kufanikiwa kutwaa ubigwa wa michuano hiyo kwa kufanikiwa kuifunga Ufaransa goli moja kwa sifuri goli lililofugwa na mchezaji Heder katika dakika 30 za nyongeza baada ya kukamilika dakika 90 za kawaida bila mshindi kupatikana.
THIERY HENRY AAMUA KUACHANA NA KAZI YA UKOCHA KATIKA CLUB YA ARSENAL.......................................
Maamuzi aliyofanya Henry ambae ni gwiji wa soka wa zamani wa club hiyo yenye maskani yake katika jiji la London nchini wingereza, ameamua kuacha kazi katika Club hiyo na kubaki kuwa mchambuzi katika kituo cha Television cha Sky sport.
Maamuzi hayo yaliyofanywa na Gwiji huyo yamewafurahisha baadhi ya viongozi wa club hiyo ya Arsenal..
Ijumaa, 8 Julai 2016
MAMIA YA WATU WATAPIGWA PICHA ZA UTUPU KATIKA MJI WA HULL NCHINI UINGEREZA.........................
![]() | |
Mamia ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherekea utamaduni katika mji wa Hull, uingereza. |
washiriki watapakwa rangi ya samawati jumamosi na kisha wapigwe picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa nampiga picha spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya sanaaa ya Ferens Art Gallery.
picha zitakazopigwa zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
Tunick, anayetoka New York, amewahi kufanya kazi kama hiyo kwingine.
Amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi sydney opera House, place des Art mjini Montrel, Mexico city na mjini Munich nchini Ujerumani.
Bw Tunick amesema kazi zake'' hugusia historia ndefu ya sanaaa ya utupu''
''Mavazi ni sanaa ya mtu mwingine''anasema.
Fashion ni sanaa. kwa kuondoa hilo[ mavazi] nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi wake''
Watu karibu 2000 wamejiandikisha kupigwa picha tangu wazo hilo litangazwe mwezi machi.
Baraza la mji wa Hull limesema baadhi ya barabara zitafungwa wakati wa shuhuli hiyo jumamosi asubuhi.
PAUL POGBA AKIRI KUA ANAHITAJI KURUDI KATIKA CLUB YA MANCHESTER UNITED.......
Jumatatu, 4 Julai 2016
MABASI MAWILI YA CITY BOYS YAUWA 24 MKOANI SINGIDA...
MANCHESTER UNITED WAPO TAYARI KULIPA PAUNDI MILIONI100 KWA JUVENTUS............
HAYA NDIO MANENO ALIYOYASEMA BARAKA THE PRINCE, KUMUHUSU MSANII MWENZAKE YOUNG KILLA.
![]() |
MSanii huyo ametoa maneno hayo wakati akiwa anafanya mahojiano na kituo kimoja cha redio
Hata hivyo kauli hiyo imeonekana kupokewa katika mtazamo tofauti na mashabiki wa mziki wa kizazi kipya, wengi wameonekana kumponda msanii huyo kwa kauli hiyo aliyoitoa na kusema, young kila ni msanii mkubwa na mwenye kipaji cha aina yake, hivyo Baraka the prince bado ni msanii mchanga sana katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya hivyo hawezi kushindana na young killa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)