C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Jumatano, 29 Juni 2016

ANGALIA NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA BILL NASS CHAFU POZI....................

ANGALIA NA DOWNLOAD HAPA VIDEO MPYA YA BEN PAUL MOYO MASHINE..............

SIKILIZA NA DOWNLOAD NYIMBO YA PAPA WEMBA FT DIMOND PLATNUMZ CHACUN POUR SOI

ANGALIA HAPA VIDEO MPYA YA MR BLUE FT ALLY KIBA MBOGA SABA,,,OFFICIALYNEW VIDEO OF MR BLUE FT ALLY KIBA MBOGA SABA..



CLUB YA CHELSEA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO KUKAMILISHA USAJILI WA MSHAMBULIAJI KUTOKA OLYMPIC MARSEILLE YA NCHINI UFARANSA

Club ya Chelsea yenye maskani yake jijini london nchini Wingereza ipo katika hatua za mwisho kumsajili Mshambuliaji kutoka club ya Olmpic Marseille, Batshuayi kwa ada ya Euro  million 33.
Mshambuliaji huyo ambae ni raia wa Ubelgiji anatarajia kujiunga na hiyo ya chelsea akitokea katika club ya olmpic Marseille ya nchini ufaransa,msimu uliopita mchezaji huyo alifanikiwa kuifungia club hiyo magoli 24 katika ligi ya nchi hiyo maarufu kama League one,.
Mchezaji huyo anatarajia kujiunga na mbelgiji mwenzake Eden hazard katika klabu hiyo ya chelsea katika msimu ujao.
Usajili huo ni wa kwanza kufanywa na club ya chelsea kwa msimu huu chini ya kocha mpya Antonio Conte, ikiwa ni moja ya harakati za kukiboresha kikosi cha club hiyo, kwani msimu uliopita haukua mzuri sana kwa club hiyo, iliyokua ikifundishwa na kocha  jose morinho aliyetimuliwa klabuni hapo baada ya club hiyo kupata matokeo mabaya, kitu kilichopelekea kumaliza katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu nchini wingereza na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya klabui bigwa barani ulaya katika msimu ujao.

CLUB YA LIVERPOOL YAKAMILISHA DILI LA KUMSAJILI MCHEZAJI WA SOTHAMPTON KWA KUMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MINNE.

Klabu ya liverpool  yakamilisha usajili  wa mshambuliaji  Saido Mane,kutoka Sothampthon kwa ada ya Euro million 30.
Mshambuliaji huyo kutoka club ya sothampton anakua ni mchezaji wa pili kuuzwa na club hiyo katika dirisha hili kubwa la usajili wakanza alikua ni Victor wanyama ambae alinunuliwa na club ya Totenham hospurs, yenye maskani yake jijini london nchini wingereza.
Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka minne ambao utamweka klabuni hapo mpaka mwaka 2021,usajili huo ni wa kwanza kufanywa  na klabu hiyo ya liver pool yenye maskani yake katika jiji la liverpool nchini wingereza ikiwa ni moja ya harakati za kuiboresha klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi, kwani itakumbukwa katika msimu uliopita club hiyo ilimaliza ikiwa katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu nchini Wingereza,

Jumanne, 21 Juni 2016

MHARIRI WA GAZIETI LA DIRA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA GAZETI HILO KUTOA HABARI ZISIZO ZA KWELI..

Mhariri wa Gazeti la Dira afikishwa kituo cha polisi baada ya Gazeti hilo kuandika taarifa potofu ya kuibiwa kifaru cha  JWTZ.
Tangu juzi kumekuwapo na taarifa za kuibiwa kifaru cha jeshi la wananchi wa Tanzania Zilizoripotiwa na Gazeti la Dira.
jana JWTZ imekanusha taarifa hizo na kulitaka gazeti hilo kukanusha na kuomba radhi mara moja kwa kutoa taarifa za uongo kwa uma.
Taarifa mpya leo ni kwamba jeshi la polisi nchini linamshikilia mhariri wa Gazeti la Dira kwa mahojiano zaidi.

Alhamisi, 16 Juni 2016

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA RAPPER CHID BENZ KWA SASA BAADA YA KUPATA MATIBABU................

Huu ndiyo muonekano mpya wa sasa hivi wa rapa chid Benz, aliekua akipata matibabu kutokana na kuadhiriwa na dawa za kulevya
Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya nchini afya yake imeonekana kuwa nzuri baada ya kupelekwa Sober House ambacho ni kituo kinachotoa huduma kwa watu walio adhiriwa na madawa ya kulevya , rapper huyo alikaa kituoni hapo na kupatiwa matibabu kwa mwezi mmoja na baadae kuruhusiwa baada ya afya yake kurudi katika hali ya kuridhisha,
Hata hivyo meneja wa kundi la Tiptop connection Babu tale ndiye mtu aliejitolea kwa hali na mali kuhakikisha msanii huyo anarudi katika afya yake ya kawaida na kuweza kuendelea na shuhuli zake za muziki,.
Sambamba na hilo msanii huyo baada ya kupona sasa atakua anasimamiwa  na Meneja Babu tale katiaka kazi zake za mziki kwa sasa.

WABUNGE WA CHAMA CHA MAPINDUZI[ CCM]WAPENDEKEZA KUONGEZWA KWA SHILINGI 50 KATIKA KILA LITA YA MAFUTA....

Wabunge wa chama cha mapinduzi ccm wataka shilingi 50 iongezwe katika kila lita ya mafuta nchini.
Wabunge hao wa chama hicho tawala wamefikia hatua hiyo ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu walipopinga vikali zoezi la kukatwa kodi katika fedha zao za kiinua mgongo [penssen] wakidai kua hawana fedha yoyote wanayoitegemea ili kuendesha maisha yao baada ya kuustaafu tofauti na hiyo na kuongeza kua muda wao wa kukaa madarakani ni miaka mitano peke yake.
wawakilishi hao wa wananchi katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wametoa pendekezo hilo bungeni ikiwa ni zaidi ya mwezi sasa wabunge wa vyama vya upinzani wameweka mgomo wa kuto udhuria vikao vya bunge kwa madai ya kutokua na imani na spika wa bunge hilo la jamuuri ya muungano wa Tanzania.

MUME AMUUA MKEWE KWA KUMNYONGA KWA KANGA KISA WIVU WA MAPENZI......

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rehema Tumbo amenyongwa na mumewe Raphael kazembe tena kwa kutumia khanga mkoani shinyanga kisa kikuu kikiwa ni wivu wa mapenzi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga Graiftoni mushi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na inadaiwa kuwa mwanamke huyo alichelewa kurudi na alipomgongea mumewe chumbani wanakolala hakumfungulia ndipo mwanaume huyo alipoamua kumfuata na kuanza kumpiga na kumnyonga hatimae kumsababishia mauti.
Mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio hili na mpaka sasa polisi wanaendelea na juhudi za kumsaka kokote aliko,mwenyekiti wa mtaa huo bwana Edward Mihayo anasema taarifa zilimfikia kutoka kwa wanamtaa baada ya kushuhudia maiti ya rehema ikiwa imenyongwa kwa kanga.

Jumanne, 14 Juni 2016

ANTONIO KONTE AMTAKA BEKI WA MANCHESTER UNITED MATHEO DAMIAN KATIAKA KLABU YA CHELSEA.......

Kocha mpya wa klabu ya chelsea Antonio Konte  anataka kumsajili beki wa kushoto wa manchester united Mateo Damian,
Kocha huyo mwitaliano  anaetarajia kuanza kazi rasmi katika klabu hiyo yenye maskani yake jijini london nchini wingereza, katika msimu ujao, ameonyesha dhamira ya kutaka kumsajili beki wa pembeni wa manchester united matheo Damiani, beki huyo aliyesajiliwa na klabu hiyo chini ya kocha Luis Vangal, aliyetimuliwa klabuni hapo mwisho wa msimu uliopita,na mikoba yake kuchukuliwa na kocha mreno jose morinho, anauwezekano mkubwa kutua katika klabu ya chelsea kutokana na mahusiano mazuri aliyonayo mchezaji huyo na kocha Antonio Konte,
Kwa sasa mchazaji huyo yupo nhini ufaransa na timu ya taifa ya italy katika fainali za EURO, timu hiyo ipo chini ya kocha antonio konte ambae ni kocha mtarajiwa wa klabu ya chelsea na kuwa pamoja kwa kocha huyo na beki huyo wa mashetani wekundu, huenda ukawa ni mwanya mzuri kwa kocha huyo kumshawishi Matheo Damian kutua Stanford bridger.
Usajili huyo unataka kufanyika ikiwa ni moja ya harakati za kocha huyo mwitaliano  kutengeneza safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya chelsea baada ya kuonekana kutetereka katika msimu uliopita kitu kilichopelekea klabu hiyo ambao walikua ni mabigwa wa tetezi kumaliza msimu wakiwa katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu nchini wingereza...

TMTAZAME HAPA VIDEO YA MCHEKESHAJI STAN BAKORA AKIRUDIA KUIMBA WIMBO WA RAYMOND NATAFUTA KIKI..........................

VIDEO YA STAN BAKORA AKILIIMBA WIMBO WA RAYMOND KWENYE  VIDEO HIII

ITAZAME HAPA NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA MSANII RICH MAVOCO IMEBAKI STORY...............

Jumatatu, 13 Juni 2016

AGALIA HAPA LIVE CONCERT YA MSANII FAT JOE PAMOJA NA FRENCH MONTANA WAKIWA WANA PAFORM LIVE NYIMBO YA AM ALL THE WAY UP.

ANGALIA NA DOWNLOAD VIDEO MPYA YA JAY MOE PESA YA MADAFU,DRAND NEW JOINT FROM JAY MOE PESA YA MADAFU



DONALD TRUMP ASEMA HAYA KUHUSU MAUWAJI YA WATU 50 NCHINI MAREKANI.............

Mwanasiasa wa nchini marekani Donald Trump amesema  mauaji ya watu 50 katika baa jana inathibitisha msimamo wake kwamba waislamu wapigwe marufuku kukanyaga ardhi ya marekani.

Mwanasiasa huyo amesema hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waislam.
upande wa bi clinton wakiton ambae ni mpinzani wa Donald trump katika kuwania kiti cha uraisi nchini marekani ,wametoa pole kwa waathirika wa mkasa huo papo hapo wamemtaja Trump kama mtoto anaejitweza ovyo kwa jinsi anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.
Wakati huo,huo shirika la kijasusi la FBI limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi wa jinsia moja alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS.
FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo Omar Mateen tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.
Baba Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanae kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaoendeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Naye mkewe wa zamani sitora yusufiy, amemweleza Mateen kama mtu aliyekuwa na tabia za kigomvi na kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini

Alhamisi, 2 Juni 2016

MSANII RICH MAVOCO ASAINI RASMI MKATABA WA KUFANYA KAZI CHINI YA KAMPUNI YA WCB...............

Msanii wa mziki wa kizazi kipya rich mavoko asaini rasmi katika kampuni ya WCB inayomilikiwa na mwanamuziki Dimond Platnum.
Msanii huyo wa kizazi kipya ambae ni mkogwe katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya hapa nchini, amefikia uamuzi wa kusaini katika lebo hiyo ya wasafi baada ya kuridhishwa  na uendeshwaji wa kampuni hiyo iliyochini ya msanii mwenzake Dimond platnum,
Kampuni hiyo ya WCB kabla ya kumsainisha rich mavoco ilikua tayari imeshawasainisha wasanii wengine wawili wanao chipukia ambao ni Harmonize ambae tayari ananyimbo mbili zinazofanya vizuri kwa sasa nyimbo hizo ni  Aiyola,na Bado, huku mwenzake  Raymond akiwa na nyimbo mbili pia ya kwanza inaitwa huku kwetu, na ya pili Natafuta kick.
Mmiliki wa kampuni hiyo ya WCB aliandika haya katika akaunti yake ya facebok huku akiambatanisha na picha hii "welcome rich mavoco  let us take bongo fleva to the world,, aliandika dimond platnum.
Kusainiwa kwa msanii huyo rich mavoco katika lebo hiyo  anakua ndiye msanii wa kwanza mkogwe kusainiwa na lebo hiyo ya WCB..