C E O OF BMG

Picha yangu
FOUNDER AND OWNER OF BLACK GENERATION MEDIA GROUP, JORNALIST AND BROADCASTER BY PROFESIONAL.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

ITAZAME HAPA BRAND NEW JOINT FROM CHEGE FT DIMOND PLATNUM WAACHE WAOANE

UONGOZI WA CLUB YA MADRID WAANZA KUMJADILI ZINEDINE ZIDANE.......................................

Club ya Real Madrid chini ya raisi wa klabu hiyo Florentino Peres imeanza mchakato wa kumjadili kocha wa muda wa club hiyo zinedine zidane aliyepewa timu baada ya kocha Rafael Benitez kufutwa kazi ya kukinoa kikosi hicho cha mabigwa wa UEFA champions league, wenye mskani yao katika jiji la madrid nchini Uhispania. 
Uongozi wa club hiyo umeanza kumjadili kocha huyo, ili kuangalia uwezekano wa kumpa mkataba wa kudumu wa kukinoa kikosi hicho cha real madrid,baada ya kuiongoza timu hiyo kwa mafanikio katika msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa kombe la club bigwa barani ulaya maarufu kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE......

ZIMESALIA SIKU KUMI KABLA YA KUANZA TENA KWA MSIMU WA LIGI KUU NCHINI WINGEREZA[ EPL]..........,,,,,

Zimebaki siku kumi pekee kabla ya kuanza tena kwa msimu mpya wa English premier League[EPL] ya nchini wingereza ,amabapo kwa msimu huu ligi hiyo inatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na kua na makocha wenye viwango vya juu katika ufundishaji wa soka.
Miongoni mwa makocha hao wanaotarajiwa kuleta upinzani wa hali ya juu katika ligi hiyo nchini wingereza ni pamoja na Jose Morinho wa Manchester united, Pep Guardiola wa Manchester city, Antonio conte wa Chelsea pamoja na Jorgen Klopp wa Liver pool.

CLUB YA ARSENAL YAINGILIWA NA MAHASIMU WAO KATIKA DILI LA USAJILI...............

Washika bunduki wa kaskazini mwa jiji la London [ARSENAL] wamewasilisha maombi kwenye klabu ya Valencia na West Brom, wakitaka kuwa sajili shrodran mustafi na jonny Evans.
Arsenal wamewasilisha maombi hayo, lakini hawajaweka mezani dau kwa wachezaji hao wawili.
Huenda the Gunners wakapata upinzani mkali kutokakwa chelsea ambao wameonyesha nia ya kumsajili Mustaki ambaye aliwahi kuitumikia Klabu  ya Everton.
Mkataba wa Beki huyo kutoka nchini ujerumani unaonyesha kuwa  kama kuna klabu ikitaka kumsajili inatakiwa kutoa kiasi cha paundi milioni 41, lakini Valencia wamejishusha na kuwa tayari kupokea hadi pauni million 25.
Arsenal wanahitaji kuongeza beki mpya baaada ya nahodha wao per mertasecker  kusumbuliwa na majeraha amabayo huenda yakamweka nje hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Beki huyo wa ujerumani alipata majeraha hayo wakati wa mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya RC lens, ambapo  ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

KIUNGO PAUL POGBA AMKABITHI MSANII DRAKE JEZI YA JUVENTUS YENYE JINA LAKE..................

Mchezaji Paul Pogba ameleta Headlines mpya baada ya kumkabithi msanii Drake jezi no 10 ya Juventus yenye jina la POGBA,